BURUDANI ZETU :MEET AND GREAT ILIVYOFANA NDANI YA UFUKWE WA CLUB YA JEMBE NI JEMBE JIJINI MWANZA. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 9 August 2014

BURUDANI ZETU :MEET AND GREAT ILIVYOFANA NDANI YA UFUKWE WA CLUB YA JEMBE NI JEMBE JIJINI MWANZA.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga a.k.a Joe sambamba na Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions ,Bi Johayna Kusaga ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 wakiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bwa.Ephraim Mafuru  ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo wakiwa ndani ya hafla ya Meet&Great ya Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya (watakaoshiriki tamasha la fiesta) na wadau wengine ndani ya Ufukwe wa Club ya Jembe ni Jembe,ilioko nje ya mji wa Jiji la Mwanza.

Tamasha la Serengeti Fiesta linatarajiwa kuzinduliwa leo ndani ya uwanja wa CCM Kirumba,huku Wasanii mbalimbali wakiwa wamekwishawasili tayari kwa onesho hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na Wakazi wa jiji hilo la Miamba.
 Baadhi ya Wasanii bongofleva na Wadau wengine mbalimbali wa muziki wakiwa wamujumuika kwa pamoja kwenye hafla ya meet&great iliyofanyika usiku wa kumkia leo kwenye kiota cha maraha cha Jembe ni Jembe,jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2014,pichani kulia Sebastian Maganga akiwa na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM,kwenye hafla hiyo ya Meet&Great.Pichani shoto ni B Dozen,Nikson pamoja na Millard Ayo.
Baadhi ya Wasanii watakaoshiriki tamasha la Fiesta wakiwa wamejichanganya na wadau wengine wakibadilishana mawazo na kufahamiana pia.
Millard Ayo , Ahmad Michuzi , Albert G.Sengo
Millard Ayo , Albert G.Sengo na FullshangweBlog CEO John

No comments:

Post a Comment