Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa mwenyekiti wa
Kamati ya Taifa ya kukabiliana na maafa Zanzibar akikiongoza kikao
hicho kuweka mikakati maalum ya kupambana ya ugonjwa wa Ebola endapo
utaingia katika Visiwa vya Zanzibar.
Wajumbe
wa Kikao cha dharura cha Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa
Zanzibar wakiendelea kujadili mikakati mbali mbali itakayosaidia
kujikinga na ugonjwa wa Ebola ambao tayari umeshaziathiri nchi kadhaa za
Afrika Magharibi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
***********************************
Zanzibar
imeanza mikakati maalum ya kujiweka tayari kupambana dhidi ya janga la
Kimataifa la kuibuka kwa maradhi ya Ebola endapo yataingia ndani ya
visiwa vya unguja na Pemba maradhi ambayo tayari yameshazikumba nchi
kadhaa za Afrika magharibi.
Mikakati
hiyo imechukuliwa kutokana na mazingira halisi ya Visiwa vya Zanzibar
kufungamana pamoja na maingiliano ya mara kwa mara kwa wageni kutoka
nchi mbali mbali duniani kupitia sekta ya utalii inayoingiza wageni
wengi.
Kikao
cha Kamati ya Taifa ya kukabiliana na maafa Zanzibar chini ya
Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
kilikutana kwa dharura Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kupanga
mikakati itakayosaidia kukabiliana na janga hilo.
Wajumbe
wa kikao hicho kilichotoa baraka ya kuundwa kwa kamati ndogo
itakayoratibu mikakati hiyo chini ya uwenyekiti wa Wizara ya Afya
wameelezea umuhimu wa kuendelea kutolewa elimu kwa wananchi
itakayosaidia kujikinga na maradhi hayo hatari.
Walisema
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na shirika la Bandari, mamlaka ya
Viwanja vya ndege, Idara ya Uhamiaji pamoja na taasisi nyengine
ziendeleze uchunguzi na ufuatiliaji wa wageni wote wanaotoka katika nchi
ambazo tayari ugonjwa huo umeshaathiri.
“
Utaratibu wa kutolewa elimu maalum kupitia vyombo vya Habari pamoja na
magari ya sinema kwa kamati za maafa kuanzia Taifa hadi shehia juu ya
ugonjwa huo unafaa kupewa msukumo wa dharura pamoja na kuimarisha ulinzi
kwenye bandari bubu “. Walisema wajumbe hao.
Baadhi
ya wajumbe hao walishauri kujumuishwa kwa wawekezaji vitega uchumi
mbali mbali waliopo hapa nchini ambao wana taaluma wa fani tofauti
inayoweza kusaidia mikakati hiyo.
Walieleza
kwamba utafiti ufanywe kuangalia sifa za wawekezaji hao ambao
huziainisha kwenye mikataba yao wakati wanapoomba uwekezaji vitega
uchumi vyao hapa nchini.
“
Tumeshuhudia baadhi ya wawekezaji hao wakati wa maafa ya kuzama kwa
meli ya M.V Spice Island kwenye mkondo wa Nungwi walivyotusaidia
kitaalamu pamoja na mawasiliano “. Alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya
watembezaji watalii Zanzibar { ZATI } Simai Mohammed.
Kuhusu
suala la ushiriki wa vyombo vya Habari katika mapambano dhidi ya
ugonjwa huo wa ebola Wajumbe hao walishauri watendaji wa vyombo hivyo
kupatiwa semina maalum zitakazosaidia katika kutoka elimu hiyo kwa
wananchi.
Walifahamisha
kwamba wapo Wahariri na hata baadhi ya mitandao ya kijamii inaopenda
kutumia matukio kama haya kueleza mambo yaliyo tafauti na uhalisia wa
matukio yenyewe.
Ugonjwa
wa Ebola uliogundulika mwaka 1976 Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya
Congo { DRC } na Sudan ni miongoni mwa ugonjwa hatari wa mripuko
unaoenea kwa kasi na kusababisha vifo vingi kwa wakati mmoja.
Dalili
kuu za ugonjwa huu ni pamoja na homa, kuumwa kwa kichwa, kuumwa kwa
misuli na viungo vya mikono na miguu, koo, kukosa nguvu za mwili na
baadaye kufuatiwa na vipele katika ngozi, macho kuwa malegevu, kwikwi na
hatimae kutokwa na damu katika tundu mbali mbali za mwili ikiwemo pua,
masikio, mdogo na ngozi.
Ugonjwa
huu wa Ebola hujichomoza baada ya virusi vyake kuenezwa kwa kupitia
mnyama kwenda kwa binaadamu na binaadamu kwenda kwa mwengine mnyama popo
akithibitika kuwa ndie chanzo kikuu cha ugonjwa huo.
Hadi
sasa hakuna dawa wala chanjo maalum inayoweza kutibu ugonjwa wa Ebola
lakini kinachofanyika kwa hivi sasa ni mgonjwa husika kupatyiwa matibabu
ya kusaidiwa kutokana na dalili zilizojitokeza.
Mripuko
wa ebola unaoendelea hivi sasa ulianza kugundulika mara ya kwanza
nchini Guinea mnamo Tarehe 21 Marchi mwaka huu wa 2014 na baadae kuenea
kwa kasi katika nchi jirani za Liberia, Siera Leone na Nigeri.
Hadi
kufikia Tarehe 11/8/2014 jumla ya wagonjwa 1,975 wamegunduliwa
kuambukizwa ugonjwa huo wakiwemo wafanyakazi wa afya 140 ambapo kati yao
wagonjwa 1,069 na wafanyakazi 80 wa afya wamefariki dunia.
Shirika
la Afya Ulimwenguni { WHO } Tarahe 8/8/82014 lililazimika kutangaza
mripuko huo kuwa ni janga la Kimataifa la Afya la Kijamii.
No comments:
Post a Comment