Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamilius Membe,
akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, huku
waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kulia) akifuatilia mazungumzo
hayo kwa pembeni, wakati wakiwa kwenye hafla ya Baraza la Idd El Fitr, Julai 29, 2014, kwenye Viwanja vya Kariamjee, Jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi kwenye Baraza la Eid ElFitr, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiingia
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, akisindikizwa na
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Kassim.
Pinda akimsalimia Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi baada ya kuwasili ukumbini
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimsalimia Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Shaaban Issa Simba baada ya kuwasili ukumbini.
Pinda
akimtazama kwa furaha wakati Mwinyi akizindua kitabu kwa furaha ambacho
kimeandikwa na Sheikh Mkuu, Shaaba Issa Simba, kitabu hicho chenye jina
la Al Muhtaswar ni makusanyo mbalimbali ambayo sheikh Mkuu huyo
ameyakusanya na kisha kutengeneza kitambu kwa ajili ya kukisambaza
nchini kote kusaidia waislam kuzingatia vyema dini hiyo. Pamoja na wadau
kadhaa, Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe amechangia kuwezesha
uchapishaji wa kitabu hicho.
Mtoto wa jijini Dar es Salaam, Arafat Msham akiduusu kitabu hicho
Membe, Dk. Salim na Sumaye wakisoma kitabu cha Sheikh Mkuu Shaaban Issa Simba
Pinda akitoa hotuba yake kwenye Baraza hilo la Idd
Kinamama kwenye Baraza hilo la Eid ElFitr
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa na Mama Shamim Khan kwenye Baraza hilo la Eid
Mwanazuoni akighani kaswida maalum kwenye Baraza hilo la Idd
Wanazuoni wakitumbuiza kaswida kwenye Baraza la Idd |
Ustaadhi Mroki Mroki wa Habari leo akifuatilia kwa makini shughuli za hafla hiyo ya Baraza la Eid
Baadhi ya Wasanii maafurufu wa Bongo Movie akiwemo Steve Nyerere nao walihudhuria Baraza hilo
Membe akiagana na wadau baada ya shughuli za Maulid. Picha zote na Bashir Nkoromo
No comments:
Post a Comment