Katibu
Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip I. Mpango (wa pili
kushoto) akifungua mkutano wa majadiliano baina ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan kuhusu ufadhili wa miradi
ya maendeleo kwa mwaka 2014/15. Majadiliano hayo yalifanyika Julai 25,
2014 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Fedha na yaliratibiwa na
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Wajumbe
wa mkutano wakimsiliza Mwenyekiti wa mjadala Dkt. Philip Mpango. Upande
wa kulia ni wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na upande wa kushoto ni wajumbe kutoka serikali ya Japan.
Wajumbe
kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia michango mbalimbali kutoka kwa
wajumbe wa mkutano huo. Miradi iliyowasilishwa ilihusisha Sekta za
Kilimo, Viwanda, Usafirishaji, Nishati, Maji, na Afya.
Baadhi
ya wajumbe kutoka Tume ya Mipango, Klasta ya Biashara ya Kimataifa na
Mahusiano ya Kiuchumi ambao walioshiriki kuratibu majadiliano hayo
kutoka kulia Bw. Robert Senya na Bi. Sudah Lulandala wakifuatilia
mjadala wakati wa mkutano huo.
Wajumbe
kutoka Serikali ya Japan wakichukua mambo ya muhimu wakati Mkutano wa
Majadiliano ulipokuwa ukiendelea. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa
Japan nchini Tanzania Bw. Masaki Okada.
Wajumbe
wa mkutano uliohusisha Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa
Wizara, Wakurugenzi na Wataalam wa Sekta mbalimbali wakifuatilia kwa
makini majadiliano yaliyokua yakiendelea.
No comments:
Post a Comment