Wafanyakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya
banda lao na nyuso za bashasha baada ya kunyakua tuzo ya Machapisho kwa
Umma (Mass Media na Publicity) kwa mara ya tatu mfululizo kwenye
maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyozinduliwa
rasmi jana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu Iddi
katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa,
jijini Dar. Kutoka kushoto ni Programme Coordination Specialist wa
UNAIDS, Jimmy Mbazi, Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa
Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, Programme Officer wa Shirika la
Kimataifa linalohusika na uhamiaji (IOM), Charles Mkude na Mtaalam wa
Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu.
Wafanyakazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wakiwa wameshikilia tuzo pamoja na
cheti walichotunikiwa jana wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo
yaliyopewa baraka na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sefu
Iddi.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama (wa tatu kushoto) akizungumza na mzazi aliyeambatana na watoto
wake kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwa
ajili ya kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa
Mataifa hapa nchini. Kushoto ni Amos Mtamba kijana mwenye fani ya
uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia Mpango
wa Kukuza Ajira kwa Vijana " Kazi Njenje" na anayefuatia ni Programme
Coordination Specialist wa UNAIDS, Jimmy Mbazi.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma
Ledama akifafanua jambo kwa mzazi aliyeambatana na watoto kwenye banda
la Umoja wa Mataifa kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa
Mataifa hapa nchini kwenye maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya
Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K.
Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Amos
Mtamba kijana mwenye fani ya uchoraji anayefadhiliwa na Shirika la Kazi
Duniani (ILO) kupitia Mpango wa Kukuza Ajira kwa Vijana "Kazi Njenje"
akieleza kwa mmoja wa wadau namna anavyofanya kazi zake za uchoraji
ambapo UN imempa nafasi ya kuonyesha kuonyesha kazi zake za sanaa ya
uchoraji kwenye banda hilo kwa ajili yakujitafutia soko na kuendeleza
maisha yake.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akifafanua jambo kwa wageni waliofika kwenye banda la Umoja wa
Mataifa lililopo ndani ya Karume Hall kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara
ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho wa
Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
No comments:
Post a Comment