Meneja
rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune
(mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500
mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula
iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni
meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw.
Kulwinder Singh Jheeta na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya
Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak.
Meneja
rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune
(kulia) na Meneja maswakla ya kampuni wa IPTL (Company Affairs Manager)
Bw. Kulwinder Singh Jheeta (katikati) wakikabidhi sehemu ya bidhaa
zilizonunuliwa wakati wa karamu ya chakula kwa watoto yatima wapatao 500
kutoka vituo mbali mbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa, kwa ajili
ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi
ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak, ambao waliandaa karamu hiyo baada ya
kufadhiliwa na IPTL.
Meneja
rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune
(mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500
mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula
iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni
meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw.
Kulwinder Singh Jheeta.
Meneja
maswala ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw.
Kulwinder Singh Jheeta akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500
mayatima kutoka vituo mbalimbali Dar es Salaam na Wilaya ya Kondoa
kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na
taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL.
ZAIDI
ya watoto 500 wasio katika mazingira magumu na mayatima jijini Dar es
Salaam na Wilayani Kondoa wameungana na waislam wengine duniani siku ya
Jumanne kusheherekea sikukuu ya Eid, sikukuu inayoashiria kuisha kwa
mwezi wa mfungo wa Ramadhani.
Watoto
hao kutoka katika vituo mbali mbali vya watoto yatima, walipata fursa
ya kula na kufurahia pamoja na wengine wakati wa karamu ya chakula cha
watoto yatima ililoandaliwa na taasisi ya Ai-Madinah Social Service
Trust na kudhaminiwa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power
Tanzania Limited (IPTL).
Bw.
Aidan Kaude, Meneja Rasilimali Watu wa IPTL aliejumuika na watoto hao
jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe hizo alisema kampuni yake imeona
haja ya kuisaidia Al-Madinah katika kuhakikisha kuwa watoto hao
wanaohitaji msaada pia wanapata haki ya kusheherekea wakati huu muhimu
katika maisha ya waislam wote dunia mzima.
"Tulipopata
maombi toka Al-Madinah ili kusaidia kufanikisa karamu hii, Mwenyekiti
wetu mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi aliidhinisha haraka ombi hilo na
kusema kuwa ni jambo la kheri sababu watoto hao walengwa ni mayatima na
wanahitaji msaada toka kwa kila mtu ili waweze kuishi maisha ya kawaida
kama wengine wanavyoishi licha ya kupoteza wazazi wao," alisema.
Mkurugenzi
wa Al-Madinah Social Service Trust, Sheikh Ally Mubarakà aliyeandaa
tukio hilo alisema kuwa baada ya kufanyakazi karibu na kwa muda mrefu na
makundi mengi na taasisi mbali mbali za kiislam, taasisi yake imegundua
kuwa mayatima wengi wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo ni pamoja na
ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile chakula, mavazi na malazi.
Alisema
taasisi yake iliomba msaada wa kifedha toka IPTL ili nao kuwapatia
msaada wale watoto wenye maisha magumu, nafasi ya kusheherekea na
waislam wenzao. Waislam walianza kusheherekea sikukuu ya Eid Jumatatu
kwa dhehebu la Sunni na Jumanne kwa wengine, baada ya mwezi kuonekana na
kuonesha mwanzo wa Shawwal, mwezi wa kumi wa Kalenda ya mwezi wa
kiislama.
Kuonyesha
mwanzo wa Eid na kutoa Sunnah, kwa kuyafanya yake yaliyoganya na Mtume
Muhammad, waislam wengi waliamka mapema kusali sala ya Asubuhi ya Sarat
ul-Falr.
Waslam
wanasheherekea sikukuu kwa kukusanyika pamoja na marafiki na familia,
na kuandaa vyakula vizuri , nguo nzuri kupeana zawadi na kupamba nyumba
zao. Salaam ya kawaida wakati wa sikukuu hii ya Eid Madhubuti ya "Eid
Mubarak" ikimaanisha "uwe na Eid iliyo na upendo."
No comments:
Post a Comment