MAZISHI YA MTOTO WA BOKSI : MBUNGE MHE. ABOOD NA MKUU WA MKOA JOEL BENDERA WAONGOZA MAZISHI YA MTOTO NASRA RASHID KATIKA MAKABURI YA KOLLA, MOROGORO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Wednesday, 4 June 2014

MAZISHI YA MTOTO WA BOKSI : MBUNGE MHE. ABOOD NA MKUU WA MKOA JOEL BENDERA WAONGOZA MAZISHI YA MTOTO NASRA RASHID KATIKA MAKABURI YA KOLLA, MOROGORO


Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifafanua jambo juu ya maisha ya mateso ya mtoto Nasra wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu mtoto huyo katika uwanja wa jamhuri kisha mwili wake kupelekwa katika msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa kumswalia kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kolla mkoani hapa.

Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akizungumza jambo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu mtoto Nasra katika uwanja wa jamhuri kisha mwili wake kupelekwa katika msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya sala ya kuambezi kabla ya kuzikwa katika makaburi ya Kolla mkoani Morogoro.
Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed akitoa ufafanuzi wa jambo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera wa pili kutoka kushoto, Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed wa kwanza kushoto wakiwa katika shughuli hiyo.
Jeneza lenye mwili wa mtoto Nasra likiwa wasili katika uwanja wa jamhuri ikitokea msikiti kuu wa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuagwa.
Joel Bebdera akiteta jambo na Afisa wa Ustawi wa jamii mkoa wa Morogoro Oswin Ngungamtitu kulia.

Kaka wa Nasra akiwa amejiinamia kwa kuwaza jambo wakati wa matukio mbalimbali yakiendelea.
 
Kaimu Sheikhe wa Bakwata mkoa wa Morogoro Ally Mohamed wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwaongoza waumini wa dini ya kiisla kuomba dua bara baada ya kumaliza swala ya kumswalia Nasra katika msikiti mkuu wa mkoa wa Morogoro.
 
Waumini wa dini ya kiislam wakiwa wamebeba sanduku kenye mwili wa marehemu Nasra kuelekea makaburini Kolla kwa ajili ya maziko.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini kupitia kitiki ya CCM Abdullaziz Mohamed Abood kushoto akiwaongoza wananchi waliojitokeza katika mazishi ya Nasra kubeba jeneza katika makaburi ya Kolla.
 Shughuli ya mazishi zilikuwa hivi.
Bendera akichota mchanga na kuingiza kaburini.
Abood anaye alifuatia kwa kitendo hicho.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake katika makaburi ya Kolla wakati wa mazishi hayo.Picha Zote na MTANDA BLOG.

No comments:

Post a Comment