Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa,Ramadhan Mungi akiwaonyesha maaskari feki
ambao walikuwa wakifanya utapeli katika mikoa ya Iringa na Morogoro
,kulia ni Bazil Nyakunga ambae ni mwalimu akiwa na sare za polisi na
katikati ni bossi wake Godlack Mbehale.
Askari polisi Mkoani Iringa (kushoto) akiwa na maaskari feki katika ofisi ya kamanda wa polisi |
Na Francis Godwin,Iringa
MATAPELI
washindwa kubaki njia kuu sasa waanza michepuko mipya ni baada ya
jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumkamata mwalimu aliyejifanya askari
akiwa na fullu kombati za jeshi la polisi na bossi wake aliyevalia
kiraia ambae pia ni feki na ni mmiliki wa studio eneo la Kihesa mjini
hapa.
Upo
usemi usemao kuwa usiombe likukute usilo litegemea kukukuta katika
maisha yako na ukipenda kudanganya uwe tayari kudanganywa ,hakuna
asiyepata kusikia ama kusoma habari kuhusu utapeli unaoendelea hapa
nchini kwa watu wa kada mbali mbali na mazingira yanaonyesha matapeli
hawa siku zote ni watu wanaopenda wengine yawakute na sio wao na
hata kupenda kudanganya na sio kudanganywa kama ambavyo mwalimu huyo
Bazil Nyakunga (20) ambae anatuhumiwa kutapeli wazazi wengi Iringa na
Morogoro ambao wanataka watoto wao kwenda kusomea uaskari .
Mwalimu
Nyakunga akiwa na bossi wake feki Godlack Mbehale (21) walijikuta
matatani kwa kukutwa na wasilotegemea kulipata baada ya jeshi la
polisi kuweka mtego kufuatia wananchi wengi kufika polisi kulalamikia
utapeli huo wa ajira kwa vijana wao katika jeshi la polisi.
Ramadhan
Mungi ni kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa alilitonya gazeti
hili kuwa jeshi lake lilipopata stori hiyo ya utapeli waliweka
mtego eneo la Ipogolo ambapo askari huyo feki alikuwa amepiga kambi la
kitapeli kwa kuwasanua mavumba wazazi wenye uchu wa watoto wao kuwa
mageda (ma Askari).
Alisema
kuwa vijana hao ambao mmoja Nyakunga ambae ni mkazi wa Ilula Mtua
katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ni kijana aliyepata kusoma kozi
ya ualimu mkoani Shinyanga na kuwa ndie alikuwa akijifanya na askari
polisi na muda wote alikuwa akivaa sare za jeshi hilo.
Mungi
alisema kuwa kijana huyo na mwenzake wamepata kuwaliza watu
wengi sana Iringa na Morogoro na kuwa mtu wa mwisho wamemliza kiasi
cha Tsh 900,000 na kuwa njia wanayotumia ni Nyakunga kama askari baada
ya kumpata mazazi na mtu mwinye uhitaji na ajira ya polisi amekuwa
akipiga simu kwa boss wake Bw Mbehale na kuiweka simu hiyo katika mfumo
wa Laudi spika ili mtu anayetapeliwa kupata kusikiliza vema
mazungumzo hayo.
“
Nyakunga kama askari feki baada ya kumpata mteja wa kumtapeli
amekuwa akiweka simu yake katika sauti kubwa na huyo boss wake
amekuwa akisikika akipanga gharama za mtapeliwa kulipia na baada ya
kutoa pesa wamekuwa wakiingia mitini kwa kumta ahadi feki….mfano
anapopiga simu anajifanya samahani boss naomba maelekezo ya mwisho huyu
mzazi /kijana anataka kazi anapaswa kutimiza nini kwa sasa kabla ya
kuitwa katika usaili ”.
Hata
hivyo kamanda Mungi alisema kuwa ni vema wananchi kuchukua
tahadhari juu ya utapeli huo na kuwa kazi za polisi kwa sasa
haziingizwi kwa mtindo huo na kuwa jeshi hilo lina utaratibu wake wa
kuingiza vijana ikiwa ni pamoja na kuwachucha toka sekondari kwa
kujaza fomo huku wale wa elimu ya juu upo utaratibu na wale
wanaochukuliwa kwa utaalam wao pia wanautaratibu wao na si
vinginevyo.
Alisema
kuwa hakuna usaili wa askari unaofanywa mitaani ama wilayani
hivyo vijana hao walikuwa wakifanya utapeli na ni vema wananchi
kuchukua tahadhari kubwa .
Pia
alisema jeshi lake linafanya uchunguzi ili kubaini eneo ambalo
matapeli hao walipata sare hizo za jeshi la polisi na mbinu
waliyotumia kuzipata sare hizo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani.
Hata
hivyo kwa upande wao matapeli hao walidai kuwa ni kweli wanafanya
kazi na ualimu na mmoja na mmiliki wa studio eneo la Kihesa mjini
Iringa na kuwa sare hizo walizipata kutoka kwa rafiki yao ambae ni
askari polisi aliyewatuma kuzifikisha kwa ndugu yao askari .
No comments:
Post a Comment