Viongozi wa CORD Raila Odinga (kushoto) na Moses Wetangula wakihutubia wanahabari Juni 3, 2014 jijini Nairobi. Picha/EVNAS HABIL.
Na VALENTINE OBARA
Viongozi
wa Muungano wa Cord wameapa kuendelea na mikutano iliyopangwa kufanyika
Eldoret na Narok licha ya polisi kusema hakuna usalama wa kutosha
kuandaa mikutano ya kisiasa.
VIONGOZI wa muungano wa Cord wameapa
kuendelea na mikutano iliyopangwa kufanyika Eldoret na Narok licha ya
polisi kusema hakuna usalama wa kutosha kuandaa mikutano ya kisiasa.
Kinara wa
muungano huo Bw Raila Odinga amesema hawajapokea ripoti yoyote kuhusu
ukosefu wa usalama Eldoret, na hivyo basi hawatatii agizo lililotolewa
na Gavana Jackson Mandago pamoja na kamati ya usalama katika kaunti
hiyo.
“Hatujajua kama kuna
hali ya hatari kule Eldoret…haijatangazwa kwa hivyo sisi hatujui.
Natangaza hapa kwamba tutaenda Eldoret wapende wasipende, na vile vile
tutaenda kule Ntulele na tunatarajia kupewa ulinzi inavyohitajika,”
akasema Bw Odinga.
Kulingana
naye, ni kinaya kuwa polisi wanasema hakuna usalama ilhali ni jukumu lao
kutoa ulinzi kwa wananchi wanaohudhuria mikutano kama hiyo.
“Polisi wana
jukumu la kulinda wananchi kwa mikutano. Katiba inasema tu wanafaa
kupewa notisi ili walinde wananchi katika mikutano,” akasema.
Mkutano wa Eldoret ulipangiwa kufanyika Ijumaa huku ule wa Narok ukitarajiwa kuandaliwa Ntulele Jumamosi. Chanzo Taifa Leo
No comments:
Post a Comment