MAJANGA NDANI YA JIJI LETU : TASWIRA YA MFANYABIASHARA ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI AKIJARIBU KUMUOKOA MFANYAKAZI WA DUKA LA KUBADILISHIA FEDHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 5 June 2014

MAJANGA NDANI YA JIJI LETU : TASWIRA YA MFANYABIASHARA ALIYEPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI AKIJARIBU KUMUOKOA MFANYAKAZI WA DUKA LA KUBADILISHIA FEDHA


SAMAHANI KWA PICHA HII (Mwili wa mfanyabiashara aliyejaribu kumuokoa dada mmoja aliyetaka kuibiwa na majambazi,  ukiwa umelala na kutapakaa damu kutokana na risasi walizommiminia majambazi hao)
 
 
WATU  wawili  wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti likiwemo la mfanyabiashara wa madini kupigwa risasi na watu wanaosaidikiwa  kuwa ni majambazi katika eneo la Maeda  lililopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha SACP Leberatus sabas alisema kuwa katika tukio la kwanza lilitokea mapema June moja  majira ya saa 9:15 katika endoe la mtaa wa maenad ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Benedict Gabriel mwenye umri wa miaka 58 mfaya biashara wa madini na mkazi wa Mushono alifariki dunia  mara  kupigwa risasi .

Alisema kuwa  tukio hilo  la kupigwa risasi kwa mfanyabiashara huyu wa madili lilitokea wakati marehemu Benedict Gabriel  kutaka kutoa msaada  kwa Monica Msuya  (47)  mkazi wa Mbauda mfanya biashara wa Northern Bereau de change  ambapo alikuwa akivamiwa na majambazi hao na kumpora mkoba ambao ulikuwa na shilingi 5,000,000  na kukimbilia pasipojulikana

Sabas  alibainisha kuwa  uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa monica Msuya  alitokea katika hotel ya Impala  kuchukuwa pesa  hizo  na kuelekea kazini akiwa amepanda tax ambapo mara baada ya kushuka nakufungua  mlango wa kuingia ofisini kwa ghafla alitokea kijana mmoja  na kutaka kumnyang'anya  mkoba ndipo alipoanza kupambana nae lakini kijana huyo alimpiga monika msuya makofi mawili na kumpiga ngwara kisha kuanguka chini ndipo monika alipo piga kelele na kuomba msaada  huku akiwa ameshikilia mkoba wake wenye Pesa.

“wakati sasa anapiga kelele marehemu Benedict Gabriel alijitokeza nakuanza kutoa msaada na kijana mwingine aliyebaki kwenye  pikipiki alitoa bunduki  aina ya Shortgun na kumlenga marehemu ,ambapo mara baada ya kumpiga marehemu aliaanguka  na Yule kijana alifanikiwa  kuchukuwa mkoba ule  na kukimbia wakiwa na pikipiki aina ya toyo yenye rangi nyekundu  akiwa na mwenzake aliyekuwa anaendesha toyo ile “alisema Sabas
 
Ajali ya Gari

Wakati huo huo gari aina ya Nissan minibus lenye namba za usajili T. 319 AXT limemgonga mtembea kwa miguu  ambaye ni askari  polisi  aliyefahamika kwa namba E.5921 CPL Justine (43) katika eneo la ngarenaro  jijini hapa .

Kamanda wa polisi mkoani hapa amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema kuwa miili yote ya marehemu imeifadhiwa katika katika hospitali yamkoa ya maunti meru ,huku akibainisha kuwa jeshi la polisi linaendea kuwasaka majambazi waliousika na mauaji ya Benedict Gabriel.

Aidha kamanda wa polisi alitoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri  na watembea kwa miguu kuwa makini wakiwa katika  barabara ili kuepuka na ajali za mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment