USAFI WA MAZINGIRA : DKT. GHARIB BILAL AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI MWANZA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 5 June 2014

USAFI WA MAZINGIRA : DKT. GHARIB BILAL AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI YALIYOFANYIKA KITAIFA MKOANI MWANZA

Makamu wa rais Dkt. Bilal akizungumza wakati wa Kilele cha maadhimisho ya sherehe hizo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo, Juni 5.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Wilaya ya Ilemela, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza leo, Juni 5, 2014. Katika Kilele hicho Makamu wa Rais alitoa tuzo na kukabidhi vyeti kwa washindi wa Usafi wa Mazingira kuanzia Vjiji hadi Halmashauri za mikoa mbalimbali ya nchini. 






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kikombe cha mshindi wa kwanza wa usafi wa Mazingira kwa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam, Naibu Meya wa manispaa ya Kinondoni, Songolo Mnyonge, wakati wa sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, leo Juni 5, 2014.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Maji wa Wizara ya Maji, Hamza Sadiki, wakati alipotembelea katika Banda la Wizara ya Maji katika maonyesho ya Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, leo Juni 5, 2014. Picha Zote na G sengo Blog
  

1 comment:

  1. Naomba nisaidie E-mail ya idara ya mazingira mkoa wa Mwanza.naomba nisaidie kupata Email yao kwa kunitumia kwenye Email yangu ambayo ni abellyakula@gmail.com

    ReplyDelete