Ufugaji : Kampuni ya Namaingo kugawa Sungura 600 kwa Wajasirimali , Dar es Salaam - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


17 Dec 2016

Ufugaji : Kampuni ya Namaingo kugawa Sungura 600 kwa Wajasirimali , Dar es Salaam


Na Richard mwaikenda
KAMPUNI ya Namaingo, kugawa sungura 600 kwa Wajasiriamali 2000 Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa nchini.
Mpango huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim katika mkutano na waandishi wa habari eneo la mradi huo wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam jana.
Alisema kuwa walengwa watakaonufaika na mradi huo, ni Wakulima 3000 waliojiunga katika vikundi vya ushirika 30 kutoka katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kila kikundi kina wakulima 50.
Biubwa alisema kwa kuanzia ni vikundi 20 vya ushirika vyenye Wajasiriamali 2000 ndiyo watakaogawiwa sungura leo na wengine 1000 watafuata baada ya sungura hao kuzaliana. Kila kikundi kipatiwa sungura wazazi 27 na dume watatu.
"Hadi sasa tuna vikundi 30 vya ushirika, tutaanza mradi na vikundi 20 vitakavyopatiwa sungura kama mbegu ya kuzalisha kwa ajili ya kupatiwa vikundi vingine 10 vilivyobakia," alisema Biubwa.
Alisema kuwa ndani ya miezi mitano sungura wazazi 540 watakuwa wamezaa mara tatu, hivyo kuwa na watoto 9,720. Jumla hiyo inatokana na kila sungura mzazi mmoja kuzaa watoto 6.
Alisema mpango utakaofuata ni kila mwanachama kugawiwa sungura 8 kwa ajili ya kuendeleza ufugaji na kupata kipato kitakachosaidia katika maisha yao.
Akielezea faida ya ufugaji wa sungura, Meneja wa Mradi huo, Amos Misinde alisema kuwa nyama ya sungura inahitajika sana na kwamba hadi sasa zinahitajika tani 5 za nyama hiyo kwa wiki. Sungura wakifugwa kwa uangalizi mzuri mmoja anaweza kufikisha uzito wa kilo 8 ambapo kilo moja ya nyama ni sh. 8,500.
Wanahabari walipata wasaa wa kutembezwa kwenye mabanda kuwaona sungura hao walioingizwa nchini wiki hii kutoka Kenya.
Sungura hao wapo chini ya uangalizi wa watalaamu kutoka Rabbit Republic ya Kenya, Suma JKT na Namaingo Business Agency pamona na watalaam wengine kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).
Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim (kulia) na Meneja Mradi wa Sungura wa kampuni hiyo, Amos Misinde wakionesha kwa wanahabari, Dar es Salaam jana, baadhi ya sungura 600 zitakazogawiwa leo kwa Wajasiriamali 2000. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)




Biubwa akimwingiza mmoja wa sungura kwenye banda eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam

Biubwa akifafanua jambo mbele ya wanahabari alipokuwa akielezea kuhusu mradi huo

Wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati Biubwa akizungumza nao

Meneja Mradi wa Sungura wa Kampuni ya Namaingo, Amos Misinde akionesha sungura waliokwenye mabanda tayari kuwagawia wajasiriamali leo

Mabanda yenye sungura

Sungura wanaosubiri kuwekwa kwenye mabanda

Sungura akila majani

Meneja Masidizi wa Mradi wa Sungura, Denis Rugezia akiwa na sungura tayari kumpanga kwenye moja ya mabanda

Mmoja wa wafanyakazi akiwapeleka sungura kwenye mabanda. Sungura hao wamewasili kutoka Kenya.




Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), akiwanesha wanahabari sungura dume

Mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, Richard Mwaikenda akiangalia mabanda yenye sungura

Mmiliki wa Bongo weekend blog Khadija Kalili akikagua mabanda hayo

Mmoja wa wanufaika wa mradi huo akiwa kwenye mabanda hayo

Makao Makuu ya Mradi wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam.

Post Top Ad