Rais
wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya kukanusha
uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa.
Kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) na kulia kwake n Wastara
Juma na Salama "Sandra" Salimin.
Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa tarifa ya kukanusha
taarifa za uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala
ya kisiasa. Kuanzia kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) ,
Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais
wa Wasanii wa Filamu Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na
Salama "Sandra" Salimin.
Rais
wa Bongo Movie, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya uzinduzi wa
filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kuanzia
kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Lupia (Cathy) , Katibu wa TAFF mkoa wa
Mwanza, Hussein Kimu na kulia kwa Nyerere ni Rais wa Wasanii wa Filamu
Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura, Wastara Juma na Salama "Sandra"
Salimin.
Rais wa Bongo Movie Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura (katikati)
akizugumza katika mkutanona waandishi wa habari kukanusha taarifa ya uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa.
Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu akiteta jambo na Wastara Juma mara baada ya mkutano huo.
Wastara Juma akihojiwa na Timzoo Karugira wa Azam TV. Picha na Cathbert Angelo wa Kajunason Blog.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII
tasnia ya filamu Tanzania ambao wanaunda umoja unaofahamikakama Bongo
Movie wameomba kutohusishwa na masuala ya kisiasa katika shughuli zao.
Hayo
yalisemwa na Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere kutokana na hsia za
kuhusishwa kwao katika mambo ya siasa mara baada ya kushiriki katika
uzinduzi wa filamu ya “I love Mwanza” ambayo ilizinduliwa na wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Utalii,
Lazaro Nyalandu.
Steve
alisema kuwa wao kama wakuu wa tasnia ya Filamu nchini, hawana mamlaka
ya kumtenga mtukatika shughuli zao zaidi ya kumshirikisha mtu yoyote awe
mkulima, mfanyabiashara, mwanasiasi bila kujali wa chama gani.
“Membe
na Nyalandu wameshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja
wa CCM Kirumba, wewe subiri uzinduzi mwingine kama utapata nafasi ya
kualikwa, lengo letu kubwa ni kuenea sanaa ambayo imezoeleka zaidi
mkoani Dar es Salaam, ni mafanikio kwetu,” alisema Steve.
Alisema
kuwa kitendo cha kuinadi filamu hiyo mbele ya halaiki ya watu kwenye
siku ya uzinduzi wake kilikuwa ni cha kawaida tu kwa sababu hata katika
katika nyumba za ibada mambo haya hufanyika, tulifanya wazi bila kificho
kwa sababu halikua jambo la haramu ukizingatia ni jambo lililokuwa lina
lengo la kusaidia maendeleo y asana nchini katika kukuza kipato cha
wasanii wa nchini Tanzania.
Mwenyekiti
wa Wasanii wa Filam Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura alisema kuwa Membe
hakuwa na shughuli nyingine tofauti na zaidi ya uzinduzi wa filamu.
“Ukweli
ni huu katika uzinduzi wa filamu ya Ilove Mwanza ambapo Waziri wa Mambo
ya Nje Bernad Membe ndiyo alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Membe
ametokea kuisapoti Bongo Movie siyo dhambi hivyo viongozi wengine
wajitokeze kusapoti wasanii kama jinsi alivyo Rais Jakaya Mrisho
Kikwete”, alisema Anitha.
“Tume
sikitishwa sana na kusingiziwa mambo ya uongo ambayo hayana ukweli
ndani yake na kuhusishwa na masuala ya kisiasa,” alifafanua.
No comments:
Post a Comment