MABADILIKO YA SOKOINE MARATHON 2014 : SOKOINE MARATHON ITAKUWA KILOMITA 10 BADALA YA KILOMITA 21 NA KILOMITA 2 ITABAKI KAWAIDA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 8 April 2014

MABADILIKO YA SOKOINE MARATHON 2014 : SOKOINE MARATHON ITAKUWA KILOMITA 10 BADALA YA KILOMITA 21 NA KILOMITA 2 ITABAKI KAWAIDA

Wilhelm Gidabuday ; Mratibu wa Mashindano ya Moringe Sokoine Mini  Marathon 2014.

Tunaomba radhi kwa kufanya mabadiliko ya ghafla! Hiyo ni kutokana na mashauriano kati yetu sisi waandaaji, Chama Cha Riadha Mkoa  na wanariadha wenyewe.

SABABU KUU: Imeamuliwa kwamba siyo vizuri kuwakimbiza wanariadha mbio ndefu mara mbili kwa wiki moja sababu pia kutakuwa na Ngorongoro Half Marathon April 19, 2014.

Familia imeridhia ombi letu na pia imekuwa wazo zuri kwa wanariadha wazoefu ambao wanafahamu athari za kukimbia mbio ndefu mfululizo. Pia wananchi wengi sasa wataweza kushiriki Kilomita 10.


Taratibu zingine hadi sasa zipo kama ilivyopangwa, ila namba zinasajiliwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume. Tsh: 2,000 tu kwa kusajili namba yako. ZAWADI ZITATOLEWA KWA WASHINDI.

No comments:

Post a Comment