SOKOINE MARATHON 2014 : KLABU YA HOLILI YATOA FUNGU ILI KUWEZESHA MBIO ZA KUMBU KUMBU YA SOKOINE ITAKAYOFANYIKA 12/04/2014 MONDULI ,ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Mar 2014

SOKOINE MARATHON 2014 : KLABU YA HOLILI YATOA FUNGU ILI KUWEZESHA MBIO ZA KUMBU KUMBU YA SOKOINE ITAKAYOFANYIKA 12/04/2014 MONDULI ,ARUSHA

Mratibu wa Mashindano ys Sokoine Marathon 2014 Bw. Wilhelm Gidabuday.

KLABU ya Holili Youth Athletic Club (HYAC) ya mjini Holili, mkoani Kilimanjaro, imejitosa kudhamini mbio za Sokoine Mini Marathon zinazotarajiwa kufanyika Aprili 12, mwaka huu katika Kijiji cha Monduli Juu, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.

Katika udhamini huo, HYAC imetoa sh milioni moja zitakazotumika kuchapisha namba (Bibs), 1,000 za utambulisho za wanariadha.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa HYAC, Domician Genandi, alisema kilichomsukuma kufanya hivyo ni moyo wa uanamichezo na kuongeza kuwa, kwa mwaka huu wamedhamiria kuongeza nguvu zote kuinua mchezo wa Riadha nchini.

“Nimeamua kusaidia nikiwa kama mdau, sababu lengo letu ni kuendeleza michezo Tanzania, sisi wadau tunatakiwa tuwe na mtazamo wa ushindi kama taifa na si ushindi wa klabu zetu binafsi tu, au wanariadha wetu tu, HYAC tunatambua jitihada binafsi zinazofanywa na waandaaji kumuenzi hayati Sokoine,” alisema Genandi.

Aidha, Genandi alisema kwa mwaka huu klabu yake inatarajiwa kushirikisha wanariadha wengi zaidi, ambako lengo lake ni kuhakikisha anaendeleza rekodi ya mwaka jana.

Kwa upande wake, Mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday alisema kwa udhamini huo HYAC inakuwa klabu ya kwanza ya riadha hapa nchini kudhamini mashindano yanayoandaliwa na wadau wengine wa riadha na kuongeza kuwa, katika hilo wameonesha kweli kwamba wana nia nzuri ya kuendeleza michezo hapa nchini hasa riadha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad