PICHA ZA KUPENDEZA : NDANI YA KITCHEN PARTY GALA YA DEC 2013 NA DINA MARIOS - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 14 January 2014

PICHA ZA KUPENDEZA : NDANI YA KITCHEN PARTY GALA YA DEC 2013 NA DINA MARIOS

Kuserebuka kulihusika ....
Amarula ilihusika kwa udhamini...
Asante sana wadhamini wetu Amarula Cream na wadhamini wengine clouds fm,picollo hotel,pad za HC na Cassandra.Asante wote mliohudhuria SIKU HIYO pamoja na uwepo wa mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.Maoni zaidi ya kuboresha hasa upande wa speakers ambao ndio kiungo muhimu cha hii kitu.Ikumbukwe kitchen party gala ni sehemu ambayo wanawake tunakutana kuongelea mambo yetu kama wanawake na wasichana.Changamoto za kimaisha si mahusiano pekee bali namna ambavyo tutakuwa bora kila siku katika maisha yetu ya kila siku.Mwanamke ni kiungo muhimu katika jamii ni bibi,mama,shangazi,mama mdogo,mama mkubwa,dada,shosti,wifi,mama mkwe,mtoto n.k Ndio maana tunaelimishana au kukumbushana kila siku mambo mbalimbali maana majukumu yetu ni makubwa kujitambua ni muhimu.

Pia tumekuwa tukiuliziwa DvD za event zilizopita mwakani tutajitahidi maana tunakwama kuzichapa sababu ya gharama pia uchakachuaji.

Mwakani tutaona itakavyokuwa.

kwa lolote la kujenga tuandikie womeninbalancetz@gmail.com

Arusha 2014 tutaianza na nyie mkae tayari Mungu atupe uhai na afya njema!
Tulianza mazungumzo yetu na Mama Victor ambae kawaida lazima aanze na sala.Katika somo lake mama Victor alisema wanawake wengi furaha yao inakamilishwa na vitu au watu lakini furaha ya kweli ipo kwenye NAFSI lakini kubwa zaidi tumeacha kumshirikisha Mungu awe kiongozi katika maisha yetu.
 Meza wa wazungumzaji Chriss Mauki,Aunty Sadaka amepumzika kwa sasa,na Getrude Mungai.
 Chriss Mauki kwa upande wa psychology anasema kila mtu ana namna yake anavyoitazama furaha.Mwingine anaona akipata kazi nzuri atakuwa na furaha,akiolewa na mume mwenye pesa atakuwa na furaha.Akiendesha gari kali nguo na mapambo ya gharama atakuwa na furaha na kadri anavyozidi ndivyo ambavyo anajikuta haridhiki na wala havikamilishi furaha kama alivyodhani.Wanawake karibu wote wanapenda kuwa na furaha lakini wao wenyewe wakati mwingine ndio chimbuko la maisha ya huzuni na wasiwasi.Unakuta mtu anaishi maisha ya mtu mwingine akihisi akiwa kama yule ndio atakuwa na furaha.Akiona mwenzie kapata kitu fulani yupo tayari ajinyime ajitese ili aende sawa nae.Yalizungumzwa mengi siwezi kuyamaliza hapa.

No comments:

Post a Comment