Party la Kufungua Mwaka 2014: Proin Group of Companies Katika Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka ,Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 27 January 2014

Party la Kufungua Mwaka 2014: Proin Group of Companies Katika Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka ,Jijini Dar

 Msanii wa Filamu Tanzania akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Bw. Geofrey Lukaza mara baada ya kuwasili katika sherehe hiyo ya kuukaribisha mwaka Iliyofanyika Mwishoni Mwa Wiki katika Jengo la Tranic Plaza lililopo Kinondoni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies Bw. Johnson Lukaza
 Baadhi ya Wawakilishi Wa Makampuni yaliyo chini ya Kampuni ya Proin Group Of Companies wakifungua shampeni kwenye sherehe ya kuukaribisha Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Kampuni Mama ya Proin Group of Companies iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumapili ya tarehe 26 January 2014 katika Jengo la Tranic Plaza lililopo Kinondoni.
 Wawakilishi wa Makampuni yaliyo chini ya Kampuni Mama ya Proin Group of Companies wakiwa tayari kufungua shampeni katika sherehe ya kuukaribisha mwaka 2014 iliyofanyika katika jengo la Tranic Plaza lililopo Kinondoni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited (Wa Kwanza Kushoto) Bw Geofrey Lukaza akiwa katika meza moja na Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya Kuukaribisha Mwaka 2014 iliyofanyika Katika Jengo la Tranic Plaza Mwishoni Mwa Wiki.
 Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotions Limited Bw Johnson Lukaza akigonga glasi na baadhi ya wageni waalikwa waliopo kwenye meza kuu wakati wa sherehe za kuukaribisha Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Proin Group Of Companies iliyofanyika katika Jengo la Tranic Plaza mwishoni mwa wiki
 Baadhi ya wafanyakazi wa Infinity Communication  iliyopo chini ya Proin Group of Companies wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka 2014 iliyoandaliwa na Proin Group of Companies, sherehe iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Jengo la Tranic Plaza
Baadhi ya wakurugenzi wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies wakikata keki Kama ishara ya kuukaribisha Mwaka 2014 kwenye sherehe ya kuukaribisha mwaka iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Jengo la Tranic Plaza. Picha zaidi bofya hapa>>> Josephat Lukaza

No comments:

Post a Comment