Ndoa ni Muhimu : Hayawi Hayawi Dina Marios Kapata mtu wa kumpa Love and Support, Soma Alichokiandika - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 27 January 2014

Ndoa ni Muhimu : Hayawi Hayawi Dina Marios Kapata mtu wa kumpa Love and Support, Soma Alichokiandika


Happy new year wapenzi wangu woteee ni muda sijaongea nanyi hapa kwenye blog lakini wapo ambao naongea nao kwenye simu kila siku tukijuliana hali na kutakiana amani na upendo katika maisha haya tunayoishi.Mungu ni mwema tulifanikiwa kufunga mwaka 2013 na kuukaribisha 2014.Na bado tunaendelea kumuomba na kumshukuru aendelee kutusimamia na kutupigania kwani tunaweza mambo yote katika yeye atutiae nguvu.
Kiukweli mwaka 2013 kwangu ulikuwa wa baraka tele sina malalamiko yoyote zaidi ya kushukuru kwa hali zote nilizopitia.Kwa kazi ninayofanya nakutana na watu mbali mbali ambao pengine wamekata tamaa ya maisha kwa wingi wa changamoto zinazowakabili kimaisha na mimi kuona nimebarikiwa sana hata kama kuna jambo nalitamani kulipata sitalalamika kwa nini sina?bali ntaendelea kumuomba Mungu aendelee kunibariki.
Nimekaa muda kimyaa maswali yakawa mengi kuhusu mie kuwa mjamzito.Sikutaka kuzungumza hapa ili kukidhi kiu ya udaku kwa yule alokuwa akihoji tena wengine walikuwa wakituma comments na kashfa juu.Niliamua kukaa kimya nideal nalo mimi mwenyewe personal.Kama ulishawahi kusoma nilichowahi kuandika hapa http://dinamarios.blogspot.com/2013/05/maisha-bila-mama.html
nilielezea maisha yangu ya nyuma yalivyofanya niwe muoga wa kuwa mama au kuolewa kama hukusoma ingia hapo usome.
Kwa hiyo hili lilipotokea nilihitaji love and support ili kusimama na kuamini kila kitu kitakuwa sawa.
Nashukuru Mungu nimepata hivyo vyote kutoka kwa mhusika mkuu.Anaitwa Reuben Ndege sio meneja wa skylight band kama walivyandika wadaku na wadakuzi.Amenipa love and support kwa kila hali.Tumekuwa wapenzi kwa miaka mingi sana lakini kama ujuavyo mapenzi ya ujana off and on zisizoisha kuvurugana kila leo.Ila sasa tupo pazuri.
Familia yangu pia baba yangu Mzee Peter amekuwepo na mimi bega kwa bega maana ndio baba ndio mama kwangu.

Namshukuru Mungu nimezungukwa na upendo na amani hilo ndio kubwa nililokuwa nahitaji.Kuna mliokuwa mnasema sijiu najificha,naona aibu,sijui sijiamini.Sasa ina maana siendi kazini?siendi hospital/clinic?siendi bank?shopping nipo tu nimejificha?
Kila mtu ana namna yake ya kudeal na vitu kwanza hata picha napiga basi sizipendi,sipendi simu wala computer naona vinanivuruga.
Kuna marafiki zangu ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu kwa hali yoyote sio ile ambayo ipo confortable kwao.Maana kuna marafiki watakuwa karibu na wewe wakati ule unaweza kwenda club huku na kule ukiwa katika hali nyinginge hawakutafuti na hawana mpango na wewe.Utakesha wewe ukiwatafuta ukihisi ni wenzako kumbe siku nyingi walishakudelete.Nawashukuru sana
Fide Mwakitalima,Asma Makau,Queen Geofrey,Sophy,Vida Nassari,Zamaradi,Gea Habib yaani naongea nao kila siku since day 1 wakinishauri hili na lile hata iwe usiku mwingi wapo kwa ajili yangu.
Kupitia leo tena hapa kwenye blog nina mama zangu,dada zangu,aunt zangu na kaka zangu ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu hata bila ya mimi kuwafahamu.Kila siku asubuhi mpaka usiku naongea nao kwa simu mpaka nahisi kama nawafahamu.Wamekuwa sehemu ya maisha yangu ni wengi siwezi kuwataja hapa.Ni upendo wa pekee kwa kweli mpaka wakati mwingine naogopa.
Mwaka huu mpya mie kwa sasa nimeuanza nikiwa nyumbani nimeanza likizo sipo kwenye leo tena.Sasa hata vya kublog sivioni,nikijaaliwa ntakuwa naandika vile ninavyoviona katika mazingira niliyopo sio ya ofisini.
 
Haya wapenzi kama kuna malengo hatukutimiza mwaka jana tuongeze juhudi zaidi kuyafikia mwaka huu....amani kwenu wote!. The CEO wa Blog ya Wazalendo 25 Blog  Gadiola Emanuel anakupongeza kwa hatua uliofika, Mungu akutangulie...

No comments:

Post a Comment