MATUKIO YA MAZISHI : JK AONGOZA WANANCHI WA MIONO KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, MHE. RAMADHAN BWANAMDOGO. - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Monday, 27 January 2014

MATUKIO YA MAZISHI : JK AONGOZA WANANCHI WA MIONO KATIKA MAZIKO YA ALIYEKUWA MBUNGE WA CHALINZE, MHE. RAMADHAN BWANAMDOGO.


 Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia . Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Miono wakati wa shughuli za maziko.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge huyo yamefanyika kijijini kwao Miono.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiweka udongo kaburini.
 Askari wa Bunge wakibeba jeneza kuelekea kaburini wakati wa maziko.
 Viongozi wakijumuika na waombolezaji makaburini.
 Waombolezaji wakishiriki kuomba dua nyumbani kwa marehemu. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment