Rais Jakaya Mrisho Kikwete na
Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea
Marekani katika ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda huku Makamu wa Rais Dkt
Mohamed Ghalib Bilali akiangalia wakati alipowasili katika Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini wakati alipowasili
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Wanaofuatia ni Mbunge wa Nkenge Mhe. Asumpta Mshama na Mbunge wa Wawi
Mhe Hamad Rashid Mohamed.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Rita Mlaki alipowasili
katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam akitokea Marekani katika ziara ya kikazi.
Picha na IKULU
----
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amerejea nchini mchana
wa jana Jumatatu, Septemba , 2013, baada ya ziara ya kikazi yenye mafanikio
makubwa katika Marekani na Canada.
Imetolewa na:
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Miongoni mwa shughuli
nyingine nyingi katika ziara hiyo, Rais Kikwete alihutubia Kikao cha 68 cha
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN)
mjini New York.
Rais Kikwete ambaye
aliondoka nchini Jumapili ya Septemba 15 alianzia safari yake mjini San
Francisco, Marekani, ambako miongoni mwa mambo mengine alizindua Ubalozi Mdogo
wa Tanzania katika Jimbo la California.
Rais pia alikutana na
kuzungumza na Jumuia ya Watanzania katika Jimbo hilo na kukaribishwa katika
Jiji la Vallejo katika sherehe za miaka 20 za uhusiano wa kimji kati ya Jiji
hilo na mji wa Bagamoyo.
Ziara ya Rais Kikwete
San Francisco ilifuatiwa na ziara ya mjini Washington ambako shughuli zake
kubwa zilikuwa kukutana na viongozi wa Bunge la Marekani na pia kuhudhuria
Hafla ya Chakula cha Usiku cha Taasisi ya Kulinda Hifadhi na Mazingira ya Bunge
la Marekani (ICCF) ambako alitunukiwa
tuzo maalum za Mtunzaji Mazingira Bora wa Mwaka.
Aidha, Rais Kikwete
alishuhudia utiaji wa saini mikataba ya kufungua Ofisi Ndogo za Ubalozi wa
Tanzania katika majimbo mbali mbali ya Marekani.
Baada ya hapo, Rais
Kikwete alikwenda Canada ambako alitunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa
Sheria na Chuo maarufu na kikongwe cha Canada cha Guelph ambacho ni maarufu
duniani kwa shughuli na utafiti wa kilimo.
Kufuatia ziara hiyo ya
Canada, Rais Kikwete alikwenda New York ambako alikuwa na shughuli nyingi ikiwa
ni pamoja na kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la UN Ijumaa ya wiki iliyopita, akakutana na Katibu Mkuu wa UN Mheshimiwa Ban Ki Moon, akashiriki
kikao maalum cha wakuu wa nchi kujadili hali ya Mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo (DRC)
kilichoitishwa na Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Akiwa mjini New York,
Rais Kikwete pia alikuwa kiongozi pekee wa Afrika aliyealikwa kushiriki katika
Mkutano wa Rais wa Marekani Mheshimiwa Barack Obama na taasisi zisizokuwa za
kiserikali duniani na pia alihudhuria Halfa Maalum iliyoandaliwa na Rais Obama
alipomaliza kuhutubia Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la UN.
Aidha, Rais Kikwete
alishiriki Mkutano wa Mwaka wa Taasisi ya Clinton
Global Initiative na pia akawa mzungumzaji rasmi katika Mkutano wa
Kupambana na Ujangili Duniani uliotishwa na Rais Ali Omar Bongo Ondemba wa
Gabon.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
30 September 2013
No comments:
Post a Comment