Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiingia ndani ya Uwanja wa
CCM Kirumba kwa maandamano ya kufunga maadhimisha Wiki ya Nenda kwa
Usalama Barabarani leo. Maadhimisho ya Nenda kwa Usalama yamefungwa
na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge baada ya
kufunguliwa mwanzoni mwa wiki hii na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk Emmanuel Nchimbi. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama
na Mazingira kutoka Makao Makuu ya Wakala wa Barabarani Tanzania (Tanroads), Zafarani Madayi akitoa maelezo
kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge
(wapili kushoto) jinsi Tanroads inavyoweza kutengeneza barabara bora
na zenye alama za usalama kwa lengo la kuondoa ajali mbalimbali zinazoweza
kutoa barabarani kabla ya kuyafunga maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika
katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Watatu kushoto ni Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama
Barabarani, Pereira Ame Silima. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu
ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Maneja Masoko wa Shirika la Bima la Taifa (NIC),
Elisante Maleko akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara
ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (wapili kushoto) ya jinsi ya shirika
hilo linavyotoa bima za magari, mali, maisha na afya wakati alipokuwa
analitembelea banda la shirika hilo katika maonesho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani kabla ya kuyafunga maonesho hayo yaliyokuwa yanafanyika
katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kushoto ni Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama
wa Barabarani, Pereira Ame Silima. Kulia ni Afisa Bima wa shirika hilo
Hollo Kazi. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI
UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima akitoa
hotuba fupi leo ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya
Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge (watatu kushoto) kutoa hotuba ya kufunga
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyokuwa yakiadhimishwa
Kitaifa katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza. Kulia ni Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga. Kauli mbiu
ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI,
WEWE NA SISI SOTE”.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson
Lwenge, akitoa hotuba ya kufunga Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani leo yaliyokuwa yakiadhimishwa Kitaifa katika Uwanja wa CCM
Kirumba, jijini Mwanza. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza Usalama Barabarani, Pereira
Ame Silima, kulia ni Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani,
DCP Mohamed Mpinga. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “USALAMA
BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, DCP Mohamed Mpinga, akikionesha kitabu cha taaluma
ya ufundishaji wa madereva kilichozinduliwa na mgeni rasmi Naibu Waziri
wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson Lwenge, kabla ya kufunga maadhimisho
ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyokuwa yanafanyika jijini Mwanza. Kulia
(waliokaa) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa
Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima. Kauli mbiu ya Maadhimisho
ya mwaka huu ni “USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI
SOTE”. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius Rweyunga (kushoto) akisalimiana na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama
Barabarani, Pereira Ame Silima, baada ya kupokea cheti cha kuthamini
mchango wa Radio hiyo iliyopo Dar es Salaam kwa kutangaza habari mbalimbali
za usalama barabarani. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
yamefungwa rasmi na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Gerson
Lwenge, jijini Mwanza leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni
“USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE”. Picha na
Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment