Miss
Utalii Tanzania 2013, Hadija Said Mswaga, amesema kuwa kupatikana kwa
nyati mweupe wa ajabu na pekee duniani katika hifadhi ya Ngorongoro,
imekuwa ni chachu na kichocheo cha pekee kwake katika mpango mkakati
wake wa kuitangaza Hifadhi ya Ngorongoro kitaifa na kimataifa, ambapo
kwa kuanzia ameamua kuanza kampeni hiyo kupitia mashindano ya dunia
anayokwenda kushiriki ya Miss Tourism World 2013, ambayo mwaka huu
yanafanyikia nchini Equatorial Guinea Octoba 12, 2013.
Kupatikana
kwa Nyati huyo wa ajabu Mweupe, ambaye hapatikani sehemu nyingine
yoyote Duniani, wakati huu ambao anakwenda katika mashindano hayo ya
Dunia, imekuwa ni fulsa ya pekee kwa Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro na kwake , kuithibitishia dunia kuwa Ngorongoro Cater ni
Ajabu la Asili la Dunia Barani Afrika. Ambapo sasa Ngorongoro Crater
pamoja na maajabu ya bonde lenyewe la kreta ya Ngorongoro, pia kuna
maajabu ya Nyati Mweupe, Unyayo wa Binadamu wa kale zaidi Duniani,
Mchanga wa ajabu unao hama kila mwaka kwa umbo la Nusu mwezi, Mlima
wenye Volkano Hai wa Oldonyo Lengai, lakini pia ushirikiano wa kuishi
bila kudhuriana wa binadamu na Wanyama katika hifadhi hiyo na
upatikanaji wa jamii karibu zote za Wanyama wakubwa (BIG FIVE) na adimu
duniani wakiwemo Faru Weusi,Duma,Mbwa Mwitu, Kaka kuona n.k.
Ngorongoro
Crater na Hifadhi nzima ya Ngorongoro ni tunu ya Taifa la Tanzania,
nahazina ya Dunia ambayo tunapaswa kuienzi na kuitangaza kwa nguvu zetu
zote, ili iweze kuingiza pato na kuchangia zaidi uchumi na pato la
Taifa, lakini pia kukuza na kuendeleza huduma za jamii ,ikiwemo elimu na
afya. Naupongeza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa
jitihada zao za kukuza utalii na kupambana na majangili , nawaomba
kuimarisha na kuongeza mapambano na vita dhidi ya ujangili na majangili,
ili kuhakikisha kuwa majangili hao hawamdhuru nyati huyo wa ajabu na
Wanyama wengine katika hifadhi hiyo. Lakini pia naiomba mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro kumlinda nyati huyo dhidi ya Wanyama wengine wala
nyama kama samba n.k.
Wafanyakazi
wa hifadhi hiyo Ijumaa ya tarehe 27-9-2013 asubuhi wakiwa katika basi
la mamlaka wakienda kazini walimshudia Nyati huyo akiwa na kundi la
nyati wengine kandokando ya barabara ndani ya hifadhi hiyo. Jambo ambalo
liliwavutia na dereva wa basi hilo kulazimika kusimamisha basi kutoa
fulsa kwa wafanyakazi hao kumshudia nyati huyo na baadhi yao kupiga
picha kwa simu zao na kamera walizokuwa nazo.
Hadija
ameushukuru uongozi wa Ngorongoro , kwa kumpatia DVD zaidi ya 100 ya
hifadhi hiyo,ambazo atakwenda kuzigawa kwa washiriki wote 126 na vituo
vya Televisheni vya nchi zao wanaoshiriki katika mashindano hayo ya
Dunia ya Miss Tourism World 2013 mwaka huu. Baada ya kurudi nitazunguka
nchi nzima na dunia nzima kuitangaza Ngorongoro kwa kushirikiana na
Uongozi wa Miss Tourism Tanzania Organisation na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment