Wanahabari wa vyombo mbali mbali na
wadau wa habari mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya amani
ya kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari
mkoa wa Iringa (IPC) .Picha Zote na Francis Godwin
Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari yakipita eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa.
Katibu wa IPC Francis Godwin
akiongoza maandamano ya wanahabari na wadau huku akiwa juu ya gari
na picha ya marehemu Daudi Mwangosi.
Wanahabari Iringa katika maandamano ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi.
Maandamano ya wanahabari na wadau
wa habari mkoa wa Iringa ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi
yakipita eneo ya uhindini.
Wananchi wakishuhudia maandamano hayo
Katibu wa IPC Francis Godwin mwenye
pama akikabidhi maandamano ya mwenyekiti wa IPC Frank Leonard na
wadau wengine eneo la Maktaba ya mkoa wa Iringa
Katibu wa IPC Francis Godwin kushoto
akikabidhi picha ya marehdemu Daudi Mwangosi kwa mwenyekiti wa IPC
Frank Leonard kulia,wanaoshuhudia ni mzee Fulgence Malangalila na
Majjid Mjengwa
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kushoto akikabidhi picha ya Mwangosi kwa mwasisi wa IPC mzee Fulgence Malangalila
Viongozi wa IPC kutoka kulia Francis Godwin katibu na Frank Leonard mwenyekiti na mwakilishi wa wananchi
<<<<...............>>>
MAANDAMANO
ya wanahabari mkoa wa Iringa kwa ajili ya
kumbukumbu ya mwaka mmoja
ya kifo cha
aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa
habari mkoa wa Iringa (IPC) na mwandishi wa
Chanel Ten Marehemu Daudi Mwangosi yatikisa mji wa
Iringa leo
Maandamano hayo ambayo yameanza majira ya saa 4 asubuhi katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa yamepata kuzungukakatika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa kabla ya kupokelewa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard katika ukumbi wa maktaba ya mkoa kwa mkutano wa wadau wa habari.
katika maeneo mbali mbali ambayo maandamano hayo yamepita likiwemo eneo la Uhindini , Mashine tatu, Soko kuu na stendi kuu ya mabasi ya mikoani wananchi walilazimika kusitisha shughuli zao kushuhudia maandamano hayo ambayo yaliongozwa na askari wa usalama barabarani .
Maandamano hayo ambayo yameanza majira ya saa 4 asubuhi katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Iringa yamepata kuzungukakatika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa kabla ya kupokelewa na mwenyekiti wa IPC Frank Leonard katika ukumbi wa maktaba ya mkoa kwa mkutano wa wadau wa habari.
katika maeneo mbali mbali ambayo maandamano hayo yamepita likiwemo eneo la Uhindini , Mashine tatu, Soko kuu na stendi kuu ya mabasi ya mikoani wananchi walilazimika kusitisha shughuli zao kushuhudia maandamano hayo ambayo yaliongozwa na askari wa usalama barabarani .
Akizungumza baada ya kupokea maandamano
hayo ,mwenyekiti wa IPC Bw
Leonard alisema kuwa
lengo la maandamano hayo ni kumkumbuka
Mwangosi pamoja na kutazama changamoto
mbali mbali ambazo wanahabari wamekuwa
wakikabiliana.
Alisema kuwa hakuna
mtanzania asiyetambua mchango
wa Mwangosi katika uhai
wake na kuwa kutokana na mchango wake
umoja wa vilabu
vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeanzisha tuzo maalum kwa wanahabari itakayopewa jina la Daudi Mwangosi na mshindi
atapewa kiasi cha Tsh milioni 10.
Alisema tuzo
hiyo itakuwa ikitolewa
kila mwaka na UTPC na ili
mwanahabari aweze kushinda
tuzo hiyo ,lazima apitie katika misuko
suko katika kazi hiyo ,pia
wale watakaopigania maslahi yao
na fisa nyingine
nyingi.
Hivyo aliwataka wanahabari
wanachama wa Vilabu vya
wanahabari na wale
wasio wanachama ambao
wanafanya kazi Tanzania kujitokeza
kuchangamkia tuzo hiyo.
Mbali hilo aliwataka
wanahabari kuendelea kuzingatia
maadili yao ya kazi hiyo
ili kuongeza imani kwa watanzania
.
Alisema kuwa
iwapo wanahabari watafanya
watazingatia maadili ya
uandishi Taifa linaweza
kupiga hatua katika maendeleo.
Wakati huo huo IPC
imetoa mikopo ya
zaidi ya Tsh 500,000 kwa wanachama
wake ili kuwawezesha kuboresha
zaidi shughuli zao kwa
kununua vifaa vya kazi
Marehemu
Mwangosi aliuwawa na
polisi septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji
cha Nyololo wilaya ya
Mufindi wakati wa
ufunguzi wa tawi la
Chadema kijiji cha Nyololo. Picha Zote na Francis Godwin Mzee wa Matukio Daima
No comments:
Post a Comment