MSANII WA FILAMU ELIZABETH MICHAEL 'LULU' AFUNIKA KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YAKE YA "FOOLISH AGE" KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 31 August 2013

MSANII WA FILAMU ELIZABETH MICHAEL 'LULU' AFUNIKA KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YAKE YA "FOOLISH AGE" KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM


 Elizabeth Michael Aka Lulu akitoa Shukrani kwaWadau wote waliojitokeza katika Usiku wake wa uzinduzi wa Filamu yake Mpya iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia Leo
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Proin Promotions Limited Geofrey Lukaza (Kushoto) akiwa na Waifu wake Groly Lukaza (katikakati) pamoja na Pedeshee Mamaa Ng'onzi wakijiachia Mbele ya Kamera ya Lukaza Blog usiku wa kuamkia Leo katika uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited
 Lady Jay Dee aka Anaconda akitoa Burudani katika Uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Lady Jay Dee akiwa pamoja na Machozi Band walitoa Bururdani Safi Sana katika Uzinduzi huo Uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
Msanii Barnaba akitoa burudani katika uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu uliofanya na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
 Katikati ni Mama Mzazi wa Marehemu STEVEN KANUMBA akiongea kwa furaha huku akitoa machozi na Msanii wa Filamu Tanzania Wema Abraham Sepetu(kushoto) na Rafiki yao katika Uzinduzi wa Filamu ya Lulu ulioandaliwa na kufanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
 Wema Sepetu (aliyepiga magoti) akikumbatiana na Mama mzazi wa marehemu Steven KANUMBA wakati wa Uzinduzi wa Filamu ya Mwanae Elizabeth Michael katika Ukumbi wa Mlimani City, uzinduzi uliokwenda sambamba na burudani kutoka Kwa Wasanii mbalimbali wa Muziki wa Bongo Fleva katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo.
Wadau wakisakata Mduara katika uzinduzi huo wa filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa kuamkia leo, Uzinduzi huo wa Kufa mtu uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ulifana kupita Kiasi
 Baadhi ya Wadau Mbalimbali waliojitokeza katika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Pron Promotions Limited.
Meza ya Viongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Kuanzia Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Bw Geofrey Lukaza, akifuatiwa na Pedeshee Mamaa Ng'onzi, Bwa Johnson Lukaza Mwenyekiti waa Makampuni ya Proin Tanzania, Gadna G Habash na Lady Jay Dee aka Anaconda wakiwa makini Kufuatilia Uzinduzi Mzima wa Filamu Mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited.
Paul SekaBoy Mkurugenzi Wa Sekaboyi Production akiwa na rafiki yake katika uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City Usikuwa kuamkia leo
Mmiliki wa Lukaza Blog Josephat Lukaza akiwa katika Picha ya Pamoja na Mmoja wa Watembeleaji wakubwa kabisa wa Lukaza Blog Maa Fetty katika Uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City. Picha zote na Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment