CLOUDS MEDIA GROUP WAENDELEZA SEMINA YA FURSA KWA VIJANA MKOANI MTWARA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 31 August 2013

CLOUDS MEDIA GROUP WAENDELEZA SEMINA YA FURSA KWA VIJANA MKOANI MTWARA

Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume  akizungumza kwenye semina ya FURSA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B leo,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiliwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana, pia Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA >>>

No comments:

Post a Comment