KAMPUNI YA CLOUDS MEDIA YATOA DARASA KUHUSU KUTAMBUA FURSA ZILIZOPO MKOANI KIGOMA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Saturday, 17 August 2013

KAMPUNI YA CLOUDS MEDIA YATOA DARASA KUHUSU KUTAMBUA FURSA ZILIZOPO MKOANI KIGOMA



Mkuu mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu,Mh Issa Machibya akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa Semina ya Fursa kwa vijana zinazopatikana ndani ya mkoa wa Kigoma na kwingineko,mapema leo asubuhi.Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group ambao ndio waratibu wa tamasha kubwa la burudani hapa nchini la Fiesta 2013,imehudhuriwa na vijana mbalimbali kutoka kila pembe ya mkoa huo wakiwemo na wasanii mbalimbali maarufu kutoka jijini Dar,ambao wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.Aidha katika Semina hiyo ya Fursa,baadhi ya vijana wengi walionekana kuvutiwa kwa kiasi kikubwa kwa yaliyokuwa yakizungumziwa,ikiwemo suala la ujasiliamali.
 Mkurugenzi wa Vipindi na Utafiti kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akimkaribisha mgeni rasmi wa semina hiyo,Mh Issa Machibya mapema leo asubuhi,kwenye ukumbi wa Kibo Peak,uliopo Kigoma mjini,kulia kwake ni msanii mahiri wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto ambae pia likuwa ni mmoja wa watoa mada kuhusiana na suala zima la Fursa.Semina hiyo imewashirikisha wadau mbalimbali,wakiwemo NSSF,Wasanii wa Bongofleva,wakazi  wajasiliamali mbalimbali ndani ya mji wa Kigoma.
 Pichani juu ni baadhi ya Wasanii wa Bongofleva na wadau wengine wakiwemo wakazi wa Kigoma wakisiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo kuhusiana na fursa mbalimbali. 
 Sehemu ya Meza kuu ikishangilia jambo,kutoka kushoto ni Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah,Mkuu wa Wilaya ya Uvinza ambae alikaimu pia nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Kigoma mjini,Mh.Khadija Nyembo,Mkuu wa Mkoa,Mh.Issa Machibya,Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji kutoka  Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,Msanii Mrisho Mpoto (haonekani) pamoja na msanii wa muziki wa kizazi kipya,ajulikanae kwa jina la kisanii AY.
 Baadhi ya Wasanii wa bongofleva ambao wanatarajiwa kutumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,wakitambulishwa kwa wakazi wa Kigoma,wakati wa kuanza kwa semina ya Fursa iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Kibo Peak mjini humo.
 Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa kigoma,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mji huo na wakazi wake.
Baadhi akina mama walioshiriki semina hiyo wakijadiliana jambo huku wakinukuu baadhi vipengele vilivyowagusa kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo,kushoto ni Mwana FA,Sheta,Joe Makini.
  Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akizungumza mbele ya umati wa vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa,mapema leo asubuhi.Mutahaba aliwafungua vijana wa mji huo kwa kuzichambua mada mbalimbali zilizohusu Fursa ndani ya mkoa wao,ikiwemo nini maana ya fursa,kishindo cha fursa pamoja na mada nyingine iliyohusu Fursa katika kuongeza thamani.
 Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo Peak.
 Kaimu Meneja wa NSSF mkoani Kigoma,Bwa.Said Abdallah akifafanua Fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya shirika la NSSF,zikiwemo za kujiunga na shirika hilo kurahisisha upatikanaji wa mikopo,matibabu na mambo mengine mbalimbali,aidha Bwa,Said amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha na shirika la NSSF ambako wanaweza kunufaika na huduma mbalimbali na zenye uhakika.
 Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya na mfanyabiashara,Ambwene Yesaya a.k.a AY akitoa ushuhuda wake na mifano mbalimbali  katika Semina ya Fursa,kuhusiana na fursa alizozipata na kuzifanyia kazi,na kumpelekea mafanikio aliyonayo mpaka sasa,AY amewataka vijana kutokuwa na moyo wa kukata tamaa haraka katika mambo yao wayafanyayo na pia kujali suala la muda katika mambo yao wayanayojishughulisha nayo. 
Mratibu Mkuu wa Semina ya Fursa,ambaye pia ni Mtangazaji wa Clouds FM,Gerald Hando akitoa utaratibu wa ushiriki kwa wadau mbalimbali waliojitokeza kwa wingi mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa Kibo Peak.Semina hiyo ilioonesha mafanikio makubwa kwa wakazi wa Kigoma,iliwakutanisha Wadau mbalimbali wakiwemo NSSF;Lake Oil,Wasanii wa Bongofleva na wengine wengi . Picha zote na Michuzjr-Kigoma.

No comments:

Post a Comment