MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA KANISA LA OLASITI NA KUZUNGUMZA NA WAUMINI JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

7 May 2013

MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA KANISA LA OLASITI NA KUZUNGUMZA NA WAUMINI JIJINI ARUSHA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha May 7,2013 alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani na kusababisha vifo na majeruhi.
Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti la Arusha Peddy Castelino akiomba wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipotembelea kanisa hilo May 7,2013 kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 5,2013 na kusabisha vifo na majeruhi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha, Peddy Castelino (kulia) May 7,2013 wakati alipotembelea kanisa hilo May 5,2013 ambako ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia sehemu lilipodondoshwa bomu hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa Pole Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu (kushoto ) na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Francisco Montecillo (katikati), May 7,2013 baada ya kutembelea Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha ambako May 5,2013 ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633