Ombi la kwanza la waleta rufani la
kutaka review ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa juu ya kesi ya
Mh.Lema na kutaka isikilizwe na jopo la majaji 7 limetupiliwa mbali leo
katika mahakama ya rufaa na sasa ni majaji walewale waliotoa hukumu
wamepitia ,Mahakama imetupilia mbali madai ya kwanza kwa kuwa hayapo
based on merits Kesi hii ilifunguliwa tena baada ya
Mh.Lema kushinda rufaa tarehe 21 desemba 2012,Warufani safari hii
walitaka mahakama ipitie upya uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu
na wametaka kuwe na majaji saba.
Mahakama imetupilia mbali mashtaka yao na mahakama imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.
WAKATI HUO HUO
Tovuti ya Habarimaasai inaripoti kuwa Mahakama ya Rufani imeshindwa kusikiliza rufaa ya Zombe
Mahakama
ya Rufani Tanzania hivi punde imekwama kusikiliza rufaa ya Mkuu wa
Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa
Polisi (ACP) Abdallah Zombe (pichani) na wenzake wanane baada ya
kubaini kuwapo kwa kasoro kwenye taarifa ya rufaa hiyo.
Kutokana
na hali hiyo Jamhuri imeomba iruhusiwe kufanya marekebisho, lakini
upande wa utetezi umepinga na kuiomba mahakama hiyo itupilie mbali rufaa
hiyo.
Baada ya upande wa utetezi kutoa msimamo huo sasa mahakama hiyo itatoa uamuzi siku nyingine.
Kesi ya Zombe
Zombe
na wenzake wanane walikuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya
wafanyabiashara wa madini ambao wanatoka Tarafa ya Mahenge mkoani
Morogoro.
Katika kesi hiyo Zombe na wenzake wanadawa kuwaua
Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi,
Mathias Lunko, Mbena dereva teksi Juma Ndugu katika msitu wa Pande
uliopo Mbezi Luis, Jijini Dar es Salaam.
Mauaji hayo yalifanyika
Januari 14, mwaka 2006 na awali baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam kusikiliza ushahidi wa pande zote Agosti 17, 2009, mahakama hiyo
ilisema upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.
Awali
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa Mahakama ya Rufani, kupinga
hukumu ya Mahakama Kuu, akidai Jaji Salum Massati alikosea kuwaachia
huru washtakiwa hao, akidai kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia
hatiani.
Rufaa hivyo imesikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa
Mahakama ya Rufani. Jopo la majaji hao limeongozwa na Jaji Edward
Rutakangwa, akisaidiana na Jaji Bernard Luanda na Jaji Salum Mbarouk.
Katika rufaa hiyo namba 254/2009, iliyofunguliwa mahakamani hapo Oktoba 6, 2009.
No comments:
Post a Comment