
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda akifungua mafunzo elekezi
ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo katika ukumbi wa
mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.Wizara hiyo kwa
mwaka wa fedha wa 2012/13 imeajiri watumishi wapya 30.

Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Barnabas Ndunguru akitoa maelezo kuhusu mafunzo elekezi kwa watumishi
wapya walioajiriwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13 leo katika
ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Gasper Mwembezi.

Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni
kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman
Mwasoko akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi ya siku
mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi
wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Enely Mwakyoma na kushoto ni Mkurugenzi
wa Michezo Leonard Thadeo.

Baadhi ya wakurugenzi kutoka
wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza katibu
mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati akifungua
mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo
katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene.

No comments:
Post a Comment