SUMATRA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA VYENYE THAMANI YA MILIONI 2.2 KWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA MOI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


31 Dec 2012

SUMATRA YATOA MSAADA WA VIFAA VYA VYENYE THAMANI YA MILIONI 2.2 KWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA NA MOI

 
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra),Ahmad Kilima (kulia), akimkabidhi vifaa mbalimbali na madawa Mganga Mkuu Mfawidhiwa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani kwa ajili ya wagonjwa wa haospitali hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Msaada huo umetolewa na Sumatra kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa wa Hospitali hiyo wakati wa siku hizi za sikukuu
 
Maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), wakiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ahmad Kilima (wa sita kulia),  pamoja na Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani (Aliyeshikana mikono na Mgurugenzi huyo), wakiwa na vifaa mbalimbali na dawa vyenye thamani ya sh.milioni 2.2 kabla ya kuwakabidhi wagonjwa wa Hospitali hiyo ikiwa ni kuwafariji katika kipindi hiki cha sikuukuu za mwisho wa mwaka. 
 
Ofisa Habari wa Sumatra Daud Mziray akigawa vifaa hivyo kwa wagomjwa.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Ahmad Kilima akigawa vitu hivyo kwa akina mama waliopo wodi ya wazazi.
 
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani, akiwaelekeza jambo maofisa wa Sumtra na Kaimu Mkurugenzi baada ya kuwasili hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada huo.

Na: Dotto Mwaibale
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetoa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh.milioni 2,200,000 kwa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na Hospitali za Mwanayamala ikiwa ni kuwafariji katika kipindi hiki cha sikukuu.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo mwishoni mwa wiki Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ahmad Kilima alisema Sumatra imechukua hatua hiyo kwa lengo la kuwafariji wagonjwa hao.
 
“Tumetumia fursa hii ya sikuku kushirikiana na Hospitali hizo katika kuchangia na kutoa msaada wa vifaa na madawa kwa akina mama waliopo wodi za wazazi kuwafariji” alisema Kilima.
 
Alisema hatua hiyo ni kuonesha Mamlaka kujiona inawajibu wa kuwa fanya akina mama hao ambao wapo hospitalini hapo kujisikia kuwa nao ni sehemu ya watanzania wengine ambao wako katika harakati za kujenga Taifa wakiwa na Afya njema katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa 2012.
 
Alilisema walilazimika kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI), kwa kuwa kuna majeruhi wanaotokana na ajali za vyombo vya moto ambao ni wadau wao wakubwa.
 
“Majeruhi wa ajali kwa namna moja ni wadau wetu kwa sababu ya vyombo walivyotumia wakati wakipata ajali ndio maana tukaguswa kuja kuwafariji kwa kuwapa zawadi” alisema Kilima
 
Kilima alivitaja vifaa hivyo pamoja na madawa kuwa ni dawa aina ya Fefol kwa ajili ya kuongeza damu akina mama wajawazito 100, pamba za kujihifadhi akina mama na Kanga.
 
Vitu vingine ni sabuni detal kwa ajili ya watoto, detal ya maji, nepi, mafuta ya kupaka watoto wadogo, juice, nguo za watoto wachanga, sabuni za kufulia nguo na Toilet papers

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad