Omari Salisbury wa Qway International
wanaosambaza vinywaji vya Belvedere Vodka akikabidhiwa cheti kwa
mchango wao kutambuliwa na TMH.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd - Benedicta Rugemalira akitabasamu
baada ya kupokea cheti kutokana na kampuni yake kutoa mchango mkubwa
katika kuwezesha ufanisi wa shughuli ya kuchangisha fedha kwa ajili ya
kusaidia kituo cha watoto yatima cha TMH ambapo kampuni yake Mabibo Beer
Wines & Spirits ilihusika kikamilifu kunywesha wageni.
Wanamitindo Flaviana Matata na Jennifer
Bash wakipita jukwaani na magauni yaliyotengenezwa na mbunifu wa
kimataifa Sherri Hill wakiyanadi kwa wageni kwa ajili ya kuchangisha
fedha za kusaidia kituo cha watoto yatima cha TMH.
Wanamitindo wakionyesha magauni hayo meza kuu ya wageni waalikwa akiwemo Mh. Zitto Kabwe.
Wageni waalikwa waliotia fora katika
maonyesho hayo ambao walinunua magauni ya Sherri Hill kwa shilingi
Milioni 4.8 Anitha (Kushoto) na Milioni 4 Alma ( wa pili kushoto) ikiwa
ni mchango wao katika onyesho la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala 2012.
Mwakilishi wa Mohammed Dewji Foundation
Bw. Cosmas Mtesigwa akinunua bidhaa za mnada zilizotoka kwa mmiliki wa
Kampuni ya Diamond Empowerment Fund Russel Simmons wa nchini Marekani
zenye thamani ya shilingi Milioni 5 ikiwa ni mchango wa Mohammed Dewji
Foundation kwa kituo cha watoto yatima cha TMH.
Mh. Zitto Kabwe akionyesha kitabu
'SUPER RICH' kilichoandikwa na Russel Simmons alichonunua kwa thamani ya
Shilingi Milioni 4 kama mchango wake kwa kituo cha watoto yatima
kinachoongozwa na Mwanamitindo Khadija Mwanamboka cha TMH. Kushoto ni
Mwanamitindo wa Kimataifa Mtanzania anayeishi nchini Marekani aliyekuja
na bidhaa hizo Flaviana Matata.
Mh. Zitto Kabwe na Chief Judge wa BSS Madam Ritha Paulsen katika Meza kuu.
Flaviana Matata na Eve Collection.
Mwakilishi wa Kampuni ya MeTL Cosmas
Mtesigwa (kulia) Operation Manager wa Mo Blog Johary Kachwamba na
Assistant Operation Manager Zainul Mzige nao waliokuwa miongoni mwa
wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Mabibo Beer Wines & Spirits Ltd Bi. Benedicta Rugemalira akiwa na
binti yake mmiliki wa Eve Collection.
Mh, Zitto Kabwe sambamba na msanii Linex wakichana mistari ya wimbo wa Leka dutigite katika hafla hiyo.
Hafla hiyo ilipochanganya...... Shose
Sinare naye alishindwa kujizuia na kujiunga na Mh. Zitto Kabwe na Msanii
Linex katika Lekadutigite.
Mc Evance Bukuku, Nancy Sumari, Mustafa Hassanali na Asia Idarous.
Mc Abby Plaatjes na wadau.
Flaviana
Matata akiwaonyesha wageni baadhi ya bidhaa alizokuja nazo kutoka kwenye
kampuni ya Diamond Empowerment Fund ya Russel Simmons ya nchini
Marekani ambao ni mchango wa mfanyabiashara huyo wa kimataifa kwa kituo
cha TMH.
No comments:
Post a Comment