MBUNGE WA ARUSHA MH. GODBLESS LEMA AMESHINDA KESI, SASA NI MBUNGE HALALI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 21 December 2012

MBUNGE WA ARUSHA MH. GODBLESS LEMA AMESHINDA KESI, SASA NI MBUNGE HALALI







Hukumu imeangalia haswa swala la Locus Stand ya kama waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo.imeangaliwa kwa kina na kuonekana kuwa kadiri ya pingamizi ya mawakili wa lema kimomogoro na Tundu Lissu,waliofungua shitaka dhidi ya lema hawakuwa na locus stand ya kufanya hivyo.kwa hiyo mengine yote yanakuwa null and void.hukumu haikuchukua hata nusu saa. Lema sasa ni mbunge halali wa Arusha Mjini

Lema kulia, Mbowe na Nassari wakiwa mahakamani muda mfupi kabla ya kuanza kusikiliza rufani ya mbunge huyo.

Mawakili wakiwa kwenye viti vyao wakipitia rufaa hiyo kabla ya kutoa hukumu.

Hawa ndiyo waliokuwa wamefungua kesi dhidi ya lema wakiwa katika mahakama hiyo wakisubiri kutolewa kwa rufaa ya hukumu ya kesi hiyo


Mahakamani,lissu,nassari,mwenyekiti mbowe na kilewo wakiteta na mke wa lema



Lema akianza kutoa hotuba fupi baada ya kutoka mahakamani.kulia ni joshua nassari


Vitalisi kimomogoro,wakili wa lema.huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu kuanza

Tundu lisu,mtetezi wa lema.aliingia baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa.ameshangiliwa sana




Askari wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA

Hapa Lema akiwa na Henry Kilewo wakati wa maandamano ya kutoka mahakamani kuelekea makao makuu ya Chadema, Kinondoni
PICHA ZOTE KWA HISANI YA JUMA MTANDA BLOG

No comments:

Post a Comment