Mh Waziri Mkuu aliongozana na mkewe
akisalimia na Balozi wa Tanzania nchini uingereza Peter Kallaghe mara
baada ya kuwasili Ubalozini.
Mh Waziri Mkuu akisoma kitabu cha wageni kabla ya kutia sahihi .
Mh waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na watanzania.
Mh Waziri Mkuu akifananua Jambo.
Dr Hamza akisema machache
wakati wa maswali na Majibu.
Balozi wa Tanzzania nchini uingereza Mh
Balozi Peter Kallaghe akimkaribisha Mama Tunu Pinda kabla Mh Waziri
mkuu kuongea na watanzania.
Watanzania wakifuatilia hotuba ya Mh Waziri Mkuu.
Watanzania wakimsikiliza Mh waziri Mkuu.
Mh Waziri Mkuu akisalimiana na baadhi ya watanzania baada ya mkutano.
---
Salam,
Siku ya jumanne tarehe 16.10.12 Mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo
Kayanza Peter Pinda alipata fursa ya pekee ya kukutana na baadhi ya
watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za Ubalozi wetu
zilizopo hapa jijini London ili kuongea, kufahamiana nao na kuwapa
taarifa kamili kuhusu hali ya nchi Kiuchumi, Kisiasa, Kiusalama,
Kimaendeleo na changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa letu.
Mh
Waziri Mkuu alieambatana na mkewe mama Tunu Pinda walipokelewa rasmi na
Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, wafanyakazi pamoja na maofisa kutoka
ngazi mbalimbali katika Ubalozi wetu. Kabla ya kuanza hotuba yake Mh
Balozi alichukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru watanzania wote
ambao waliojitokeza kuja kumsikiliza na kumsalimia Mh Waziri Mkuu.
Akihutubia
watanzania zaidi ya mia tatu Mh Waziri alianza kwa kuongelea hali
halisi ya uchumi nyumbani ambayo inaendelea kukua vizuri taratibu siku
hadi siku tokea Mh Raisi Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mnamo
mwaka 2005. Kutokana na twakwimu za hivi kutoka idara ya uchumi
zinaonyesha kukua kwa GDP kutoka asilimia 6.9% mpaka 7% kwa sasa ambayo
imesababishwa na upanukaji kiuchumi. Vile vile pato la wastani kwa
mtanzania wa kawaida linazidi nalo kuongezeka taratibu japokua sio kwa
kasi kubwa kama ambavyo ingetakiwa. Kwa sasa Mtanzania wa hali ya chini
anaishi chini ya dolla moja ($1.00) kwa siku.
Dira
ya Maendeleo ya Taifa 2025 imedhamiria kuwa Tanzania iweze kunyanyuka
na kuingia katika ngazi ya Kati au Middle Income Country ifikapo mnamo
mwaka 2025.
Mwaka
2011-2012 changamoto kubwa ambayo imekua ikikabili Taifa letu ni
mfumuko wa bei za vyakula hususani mahindi, Mchele, sukari ambayo
imetokana na uuzwaji wa vyakula kwa nchi jirani kama Kenya, Somali, na
Sudani ya kusini kwa bei ya ghali na kufanya gharama kuongezeka nchini.
Pia kumekuwepo
kwa njaa nchini katika wilaya ya kaskazini, kanda ya ziwa na Shinyanga
ingawaje hatua madhubuti zimeshachukuliwa ili kuhakikisha
tunajitosheleza kwa chakula na
zaidi ya hapo kuwekuwepo na mikakati mizuri itaiwezesha Tanzania kuwa
''Bread Basket kwa East Africa'' kwa kulisha sehemu nchi zingine katika
jumuiya ya Afrika Mashariki
Tatizo la umeme ambalo bado limekua sugu linasababishwa na kupanda kwa gharama za mafuta ya uendeshwaji.
Mapato
ya ndani yanazidi nayo kuongezeka mfano TRA mwaka 2000 walikua
wanakusanya bilion 64 kwa mwezi wakati sasa hivi makusanyo ni kiasi cha
sh bilion 650 kwa mwezi japokua mahitaji ya nchi ni makubwa mno kuliko
mapato yanayokusanywa. Pia mauzo ya nje nayo yanazidi ya zamani.
Uwekezaji wa ndani ya nchi ni Doller 900 ($900 ml)
Ili
kukabiliana na hizo Changamoto zinazozidi kukua siku hadi siku Tanzania
imejipanga vizuri ili kuimarisha uchumi na maendelo kwa ujumla. Mh
Raisi Kikwete amerejesha timu ya mipango inayosimamiwa Dr Mipango ambaye
ndio mtendaji mkuu ili kuhakisha mipango yote inayopendekezwa ifanyike
kama ilivyopangwa. Tanzania imeweka mipango ya muda mrefu ambayo ni
miaka kumi na tano (15) ijayo. Miaka hiyo nayo imegawanywa katika
kipindi cha miaka mitano mitano ili kutekeleza azma yake kwa ufanisi
zaidi. Mh Waziri Mkuu aliendelea kufafanua kuwa Agenda kuu ya miaka hii
mitano ya kwanza Tanzania vipaumbele vimewekwa katika sekta zifuatazo:
a) Ujenzi na upanuzi wa Miundo Mbinu kama Barabara, Reli, Bandari, Viwanja vya ndege, Nishati na mkondo wa Taifa
b) Kilimo-
Kuongeza zana za kilimo bora kama matrekta, Mbolea, mbegu bora na
kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kutumia teknolojia mpya ya kilimo
pamoja na kilimo cha umwagiliaji.
c) Kuwekeza na kujenga Viwanda ( Processin Industry)
d) Maji safi na Taka
e) Rasilimali watu
Serikali
ya Tanzania imedhamiria kuongeza megawati wa umeme toka zilizopo sasa
hivi ambazo ni megawati 600 mpaka megawati 2780 ndani ya miaka ijayo ili
kuweza kukomesha tatizo la mgao wa umeme ambalo lina gharimu taifa letu
fedha nyingi na kurudisha maendeleo nyuma. Bandari ya Dar inapanuliwa
pia ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo umeshakamilika pesa na mkandarasi
vimeshapatikani imebakia kuanza kazi.
Tanzania
kuwekua na wimbi kubwa la uwekezaji ambapo nchi nyingi za magharibi
zinakimbilia kuja kuwekeza nchini kwetu hasa baada ya kugundulika kwa
gesi, makaa ya mawe, dhahabu na Uranium nyingi.
Katika
kuhitimisha hotuba yake Mh Waziri Mkuu aliongelea hali ya kisiasa
nyumbani na usalama. Kwa ujumla Tanzania bado ni kisiwa cha amani na
utulivu kulinganisha na sehemu zingine ingawaje alizungumzia matukio
mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala,
na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha
na ya mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na
mauaji ya kutisha ya RPC Barlow Mwanza. Mh Waziri Pinda aliwaomba na
kuwasihi watanzania wote kuendelea kufuata sheria pia kuwa watulivu
manake mambo yote yamefikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo
wake. Pia aliwaushuri watanzania wasiogope kurudi nyumbani mara
wamalizapo masomo au kuwekeza zaidi nyumbani ili kuweza kujenga taifa
letu
Mwishoni
kulikuwa na kipindi kirefu cha maswali na majibu ambapo watanzania
mbalimbali walipata fursa ya kumwuliza Mh Waziri Mkuu maswali na kutoa
maoni au mapendekezo yao kuhusu kero na madukuduku.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA
Asanteni
Urban Pulse Creative wakishirikiana na Miss Jestina Blog
No comments:
Post a Comment