Na Father Kidevu Blog, Amboni Tanga
Washiriki
wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2012, juzi walikamilisha zira yao ya
Kutembelea Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Manyara, Moshi na Tanga
kujionea vivutio vya utalii katika mikoa hiyo ambapo walimalizia mkoani Tanga
kwa kutmbelea Mapango ya Amboni mkuano humo.
Warembo hao wakiwa katika mapango hayo
ya kale waliweza kujionea vitu mbalimbali ambavyo ni vya kipekee na vyakuvutia
vilivyopo katika mapango hayo ya asili ya zama za kale.
Miongoni mwa vitu vilivyopo huko kwenye
mapango hayo ni sanamu za aina mbalimbali za Bikira Maria, Maandiko ya Quran,
Daraja, sanamu za jinsia ya kike na kiume, chui, na vitu vingine mbalimbali vya
kuvutia.
Hapa ni katika eneo ambalo
linafananishwa na Mlima Kilimanjaro na hapa warembo wakipanda mlima huo
ndani ya Mapango ya asya Amboni mkoani Tanga.
Wakionesho eneo ambalo linafananishwa na daraja kwa jinsi lilivyo umbika.
Hapa warembo wakipiga picha katika
kiti cha enzi. Ni jiwe lililochongeka mithili ya sofa na ukiingia
pangoni humo inapendeza kuchukua kumbukumbu.
Eneo hili ni linafananishwa na Mlango wa kupandia ndege na hapa warembo wakipanda na kutoka nje ya pango.
Bado pango hilo la Amboni linaendelea kukua. Na hapa warembo wakiangalia moja ya vitu vinavoota kila mwaka hasa wakati wa mvua.
Hapa huna budi kuinama na huko ndani waweza kuinuka bila kugusa juu.Wanapotokea..
Warembo wakiangalia moja ya vitu vya kuvutia na hapa waliangalia mchoro wa asili wa chui aliyelala baada ya kushiba.
Hakika ukifanikiwa kupita hapa
utapita pango zimana kujionea vitu vingi. Hapa lazima utambae na wengi
hushindwa kupenya hapa. Hata Father Kidevu nilipenya na warembo
walishangaa niliwezaje kupenya kirahisi.
Ni full kushangaa kwa warembo hawa
wa Redds Miss Tanzania 2012. Hakika ni utalii wa ndani uliofanywa na
warembo hawa lakini je ni watanzania wangapi tunatalii katika maeneo ya
utalii.
No comments:
Post a Comment