Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Walioketi toka kulia ni IGP Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange, Spika wa Bunge Mh Anne Makinda.
Rais Jakaya Kikwete akiwatakia heri Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Davies Mwamunyange na wanajeshi watakaopandisha kilele cha mlima Kilimanjaro Mwenge wa Uhuru mkesha wa siku ya uhuru. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi , wa pili kulia ni Naibu waziri katika wizara hiyo Dkt Fenella Mukangara na wa kwanza kushoto ni mmoja wa wataopandisha Mwenge mlima Kilimanjaro.
Rais Jakaya Kikwete akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Fatuma Mwassa na maafisa wake baada ya mkoa huo kuibuka mshindi wa jumla wa mikoa iliyofanya vyema katika mbio za mwenge wa wingi wa miradi na maandalizi.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi mwenge wa uhuru mkuu wa majeshi Jenerali Davies Mwamunyange ambaye atawakabidhi wapandishaji mlima kilimanjaro.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa ameshikilia mwenge wa uhuru mara baada ya kuupokea rasmi kutoka kwa kikosi cha wakimbiza mwenge.
(PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment