CCM YASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR, NAPE AKABIDHI VYAKULA VYA SH. MILIONI NNE. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


24 Dec 2011

CCM YASAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR, NAPE AKABIDHI VYAKULA VYA SH. MILIONI NNE.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikabidhi msaada wa vyakula kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik , katika ofisi ya mkuu huo jana. Vyakula hivyo vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 4, vimetolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia waliokumbwa na maafa ya kafuriko yaliyosababishwa na vyua katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Nape Nnauye akizungumza na kina mama wenye watoto, ambao aliwakuta kwenye Ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, leo, alipokwenda kutoa msaada wa CCM wa vyakula kwa waliopatawa na mafuriko. Kina mama hao, Mariam Msimbi na Asha Selemani (kulia) walifika kwenye ofisi hiyo kutafuta ufumbyuzi wa ndoa zao ambapo wamedai wametorokwa na waume zao huku wakiwa na watoto wadogo.
Mape akizungumza na baadhi ya wananchi alipofika kwenye kambi maalum ya Mchikichini walikohifadhiwa waathiorika mwa mafuriko, wilayani Ilala.
"Ttunashukuru serikali imetuhudumia vizuri sisi waathirilka.. wanaolalamika ni wale wanaojichomeka ili wapate msaada wakati si wahusika.." akisema mmoja wa wazee (kulia) ambao Nape alizungumza nao kujua serikali ilivyosaidia waathirika wa mafuriko, alipotembelea kambi la Mchikichini walikohifadhiwa kwa muda waathirika hao,leo.
Nape akipata taarifa za matibabu wanayopatiwa waathirika wa mafuriko, katika kituo cha muda cha wathirika hao, shule ya msingi Mchikichini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad