WAANDISHI NA PPF : WAANDISHI NA WADAU WA HABARI WAJIUNGA NA MFUKO WA JAMII WA PPF ,JIJINI DAR - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


5 Mar 2014

WAANDISHI NA PPF : WAANDISHI NA WADAU WA HABARI WAJIUNGA NA MFUKO WA JAMII WA PPF ,JIJINI DAR

 Mwandishi wa habari, Ndg Francis Dande (wa kwanza kulia) akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa pensheni wa PPF jana  mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo uliandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF ulilenga Kuwapa elimu waandishi na wadau wa habari nchini juu ya huduma nyingine zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF.
Mwandishi wa Habari wa Kituo Cha Runinga cha ITV, Bi Fatma Almasi Nyangasa akijaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF mara baada ya mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar Es Salaam, Mkutano huo uliandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF.
 Meneja Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengele (wa kwanza kushoto) akiwapa maelekezo waandishi wa habari jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa Pensheni wa PPF jana Katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar Es Salaam mara baada ya Mkutano wa waandishi na wadau wa habari kumalizika.
 Waandishi na Wadau wa habari waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF mara baada ya kujiunga na Mfuko huo hapo jana katika ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad