Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiangalia kupitia kilengeo maalum kinachotumiwa kwenye
silaha na makomando kulengea shabaha.
Makomando
wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila
shilaha wakati wa ziara yake.
Komando
wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita
juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu
alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ
wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja
hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo
zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT
No comments:
Post a Comment