MSAADA WA FEDHA : UBELGIJI YAIPA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILONI 40 KUSAIDIA SEKTA YA KILIMO NA MAJI - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


13 Mar 2014

MSAADA WA FEDHA : UBELGIJI YAIPA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILONI 40 KUSAIDIA SEKTA YA KILIMO NA MAJI

01 (1)Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile (kulia) akisaini mkataba wa msaada ambao serikali ya Ubelgiji imetoa Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 za Kitanzania kuisaidia Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano Peter Moors akimwakilisha Waziri wa Ushirikiano kwa niaba ya Serikali ya Ubelgiji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
02 (2)Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwalile (kulia) kwa niaba ya serikali ya Tanzania akikabidhiana hati walizosainiana na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Ushirikiano Peter Moors (kushoto) kwa niaba ya serikali ya Ubelgiji hivi karibuni jijini Dar es salaam.
03 (2)Baadhi ya wageni na waandishi wa habari waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa serikali ya Ubelgiji kuisadia Tanzania Euro milioni 20 sawa na sh.bilioni 40 hivi karibuni jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Eleuteri Mangi – MAELEZO)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania imepokea msaada wa jumla ya Euro milioni 20 ambazo ni sawa na sh. Bilioni 40 za Kitanzania uliotolewa na serikali ya Ubelgiji kuisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi ya kilimo na maji. 
Lengo la msaada huo wa serikali ya Ubelgiji kwa serikali ya Tanzania ni wa kusaidia sekta ya kilimo na maji kwa kuzingatia kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu na maji ni uhai kwa maendeleo endelevu taifa. 
“Napenda kuihakikishia serikali ya Ubelgiji kuwa msaada walitupatia utatumika kwa manufaa ya watanzania wote kwa malengo yaliyokusudiwa” alisema Dkt. Likwalile. 
Akisisitiza juu ya msaada huo Dkt. Likwalile alisema kuwa msaada ho umekuja muda muafaka ambapo Tanzania inatekeleza Mpango wa Maendeleo Makubwa Sasa (BRN) ambapo una manufaa ya kurekebisha  huduma za jamii ikiwemo kuwapatia wananchi maji safi na salama. 
BRN ni dhana inayotekelezwa na serikali na kuonekana matokeo yake ni mazuri katika nchi nyingine. 
Miongoni mwa watakaonufaika na msaada huo ni wakazi wa Dar es salaam. Kigoma na meneo ya vijijini na kuwapunguzia muda wa kutafuta maji umbali na muda mrefu na hivyo kuwapa nafasi ya kutumia muda wao katika shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii na kupunguza umasikini kwa maendeleoya taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mwakilishi wa Serikali ya Ubelgiji alisema kuwa uliotiwa saini ni kiashiria na alama ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya serikali nhizi mbili. 
Kwa kudhihirisha Moors alisema kuwa serikali yake pia inasaidia asisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali. 
Asasi zinazonufaika na misaada inayotolewa na serikali ya Ubegiji ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA, Chuo kikuu cha Nelson Mandela, Chuo Kikuu cha Mzumbe, VECO, DON BOSCO na TRAIAS. 
Mkataba uliosainiwa ni wa muda mfupi kwa miaka miwili 2014 hadi 2015ambao ni wa mpito ambapo unaandaliwa mpango wa muda mrefu ambao ni wa muda mrefu kuanzia 2015/2016 hadi 2019/2020

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad