Na Frida Maganga,Arusha
Watumishi na waajiriwa wa Halimashauri ya jiji la Arusha wametakiwa kufanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu na sharia pamoja na miongozo yao ya kazi pasipo kutengeneza mazingira yoyote yale ya kumwonea mwanachi yoyote yule mkazi wa mkoa wa Arusha .
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Kenani Kihongosi wakati akizungumza na wamiliki na watumishi wa Salooni kike na kiume jijiini Arusha wakati akijibu malamiko ya mmiliki wa saluni Bi Rose Barage.
Ambapo Bi. Rose aliamueleza mkuu mkoa kuhusiana na manyanyaso anayo yapata pamoja kutoka kwa mtu aliyetambulika kwa jina la Lusekelo anayetambulika kama mmiliki aliyekodisha chumba cha biashara halimashauri ya jiji la Arusha na Kumpangishia yeye kwa bei kubwa.
Kutokana malalamiko hayo mkuu wa mkoa Mhe. Kihongosi alimwagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha kuhakikisha wanampatia siku hii ya leo mkataba Bi. Rose ili aondokane na manyanyaso .
No comments:
Post a Comment