Matukio : Waziri Kikwete atua Geneva kushiriki Mkutano wa 113 ILO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Wednesday, 4 June 2025

demo-image

Matukio : Waziri Kikwete atua Geneva kushiriki Mkutano wa 113 ILO


Ataeleza utekelezaji wa nchi kuhusu viwango vya kimataifa vya kazi na Ajira 

WhatsApp%20Image%202025-06-04%20at%2014.38.06
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amewasili Jijini Geneva Uswisi kushiriki Mkutano wa 113 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) .

Katika Mkutano huo, Mhe. Ridhiwani ataeleza utekelezaji wa nchi kuhusu Viwango vya Kimataifa vya Kazi na Ajira za Kazi na kuungana na nchi wanachama kujajadili utekelezaji wa mpango kazi na bajeti ya uendeshaji wa Shirika hilo kwa mwaka 2026/27.
WhatsApp%20Image%202025-06-04%20at%2014.38.07Kuelekea mkutano huo, Mhe. Ridhiwani tayari ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi na kukutana na Mhe. Balozi Dkt. Abdallah Possi ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Jijini Geneva Uswisi na Mhe. Balozi Dkt. Hoyce Temu pamoja na watendaji wa Ubalozi huo. 
WhatsApp%20Image%202025-06-04%20at%2014.38.08 Katika hatua nyingine, ametumia fursa hiyo kumpongeza Balozi kwa kazi nzuri zinazofanywa na Ofisi hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa namna nchi itakavyoshiriki vema katika mkutano wa ILO.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *