Michezo : Simba Yashindwa Kufurukuta Ugenini ,Yapigwa 2 -0 na Al Masry - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 3 April 2025

demo-image

Michezo : Simba Yashindwa Kufurukuta Ugenini ,Yapigwa 2 -0 na Al Masry

Fadlu

 
KLABU ya Simba imeshindwa kutamba ugenini katika hatua ya robo fainali mkondo wa kwanza dhidi ya Al Masry ya nchini Misri baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Suez nchini humo.

Katika mchezo huo licha ya kuutawala mchezo kwa kiwango kikubwa, Simba haikufanikiwa kupata bao katika nafasi nyingi walizozitengeneza kupitia kwa nyota wao, Ateba, Auoa pamoja na Mpanzu.

Al Masry walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 16 ya mchezo kupitia kwa Deghmoum na kufanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Simba waliendelea kulisakama lango la Al Masry bila mafanikio huku Al Masry wakitumia nafasi hiyo kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kufanikiwa kupata bao la pili baada ya kipa wa Simba Sc kufanya harakati za kuokoa krosi na kuwafanya Al Masri kupata baodakika ya 89 ya mchezo.

Simba Sc itasubiri kufanya maajabu katika mchezo wa marudio ambao watakuwa nyumbani Aprili 9,2025 huku ikiwataka kwenye mchezo huo kushinda zaidi ya mabao mawili waweze kufuzu hatua inayofuata.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *