· Wakulima washukuru kuondokana na makato, kufungiwa akaunti
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imetambulisha kampeni yake ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ kwa wakulima wa mazao mballimbali ikiwemo Kahawa na ufuta kwenye mikoa ya Songwe na Mbeya ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kupitia uchumi jumuishi unaochagizwa na huduma rasmi za kifedha.
Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw. Mbwana Kambangwa, huku pia ikihushisha uwepo wa wadau mbalimbali wa sekta za kilimo na ufugaji kutoka mikoa hiyo miwili wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika vya wakulima na wafugaji (AMCOS), pamoja na wadau wengine wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hiyo muhimu.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa aliwaongoza maofisa wengine wa benki hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo inayotoa fursa kwa wakulima na wafugaji wa mikoa ya Songwe na Mbeya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato ‘Laptops’
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw Kambangwa pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa jitihada zake endelevu zinazolenga kuwasaidia wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ukiwemo mkoa wa Songwe, alisema ujio wa kampeni hiyo kwenye mikoa hiyo utasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa wadau mbalimbali wa sekta hizo hususani kupitia huduma mbalimbali za kibenki zilizobuniwa mahususi kwa makundi hayo ikiwemo elimu ya kifedha na huduma za mikopo rafiki.
“Ubora zaidi wa kampeni hii unaonekana pale inapohusisha utoaji wa elimu ya nidhamu ya fedha miongoni mwa wakulima mmoja mmoja na vyama vya ushirika hatua ambayo itawajengea uwezo wa kuona umuhimu wa kujiwekea akiba, umuhimu wa kutumia bima mbalimbali ikiwemo bima ya afya, bima za kilimo pamoja na kuwekeza kwenye zana za kisasa za kilimo.’’
“Hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha wakulima wetu kugeukia huduma rasmi za kifedha na hivyo kuchochea uchumi jumuishi. Hii ni hatua kubwa sana ikilinganishwa na tulipotoka miaka kadhaa iliyopita ambapo wakulima na wafugaji walikuwa hawaaminiki na taasisi za kifedha kutokana na kutokuwa waaminifu na wengine kutokuwa na dhamana.’’ Aliongeza.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo inayotarajiwa kuhitimishwa Juni 15 mwaka huu, Bw Urassa alisema walengwa wa kampeni hiyo ni wakulima wa mazao mbalimbali hususani Kahawa na Ufuta kupitia vyama vya msingi, vyama vikuu vya ushirika na mkulima mmoja mmoja ambao wanahudumiwa na benki hiyo.
Kwa mujibu wa Bw Urassa, ili mkulima mmoja mmoja ashinde zawadi ya pikipiki anatakiwa kwenye akaunti yake awe na fedha kiasi kisichopungua Mil 5 na kwa upande wa AMCOS na vyama vikuu vya ushirika zinatakiwa kuhifadhi kwenye akaunti zao za NBC Shambani fedha kuanzia kiasi cha Sh. Mil 5 hadi mil 50 ili kujishindia laptop na kuwa na fedha kwenye akaunti zao kiasi kisichopungua Sh. Mil 50 ili kujishindia pikipiki.
“Lengo la kampeni hii ni kuwahamasisha wakulima na wafugaji kutunza fedha zao kwenye mifumo rasmi ya kifedha hasa benki badala ya kutunza kwenye mifumo isiyo rasmi. Tunawakaribisha sana kufungua akaunti zao za NBC Shambani ili wawe kwenye nafasi ya kushinda zawadi hizi’’ Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao, Makamu Mwenyeki wa AMCOS ya Mwanjelwa, iliyopo wilayani Mbozi, Bw Imani Luvanda alisema kwa kiasi kikubwa wakulima wilayani humo wamekuwa wakiumizwa sana na gharama za makato ya uendeshaji wa akaunti zao za benki pamoja na kufungwa kwa akaunti zao pindi zisipotumika kwa muda kitu ambacho kimekuwa kikisababisha wengi wao kupoteza imani na matumizi ya taasisi rasmi za kifedha.
“Ila sasa kilichotuvutia zaidi kwenye akaunti hii ya NBC Shambani ni kwamba haina makato yoyote ndio kwanza mkulima anapata faida na zaidi haifungwi kiurahisi hadi ipite miaka miwili.Hii kwetu ni habari njema na binafsi takuwa balozi wa kuwaelimisha wenzangu kuhusu kampeni hii na faida za akaunti ya NBC Shambani’’ alisema.

Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, (alieshika mkasi) akijipongeza sambamba na wadau wengine mara baada ya kuzindua kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe. Wengine ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (katikati) na wadau mbalimbali wa kilimo kutoka mikoa ya Songwe na Mbeya.

Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, (katikati) sambamba na wadau wengine wakionesha zawadi za pikipiki na kompyuta mpakato ‘laptops’ zitakazotolewa kwa washindi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe. Wengine ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (wa pili kulia) na wadau mbalimbali wa kilimo kutoka mikoa ya Songwe na Mbeya.

Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Tunduma Bw Shedrack Mpanda (pichani) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Songwe Bw Joseph Jerome (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Songwe Bw Daniel Msyaliha (kulia) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.
Maofisa mbalimbali wa benki ya NBC wakiwasilisha mada mbalimbali kuhusu huduma tofauti zinazotolewa na benki hiyo mahususi kwa wakulima sambamba kuwajenga uelewa kuhusu elimu ya fedha wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, huku pia ikihushisha uwepo wa wadau mbalimbali wa sekta za kilimo na ufugaji kutoka mikoa hiyo miwili wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika vya wakulima na wafugaji (AMCOS), pamoja na wadau wengine wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hizo.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), imetambulisha kampeni yake ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ kwa wakulima wa mazao mballimbali ikiwemo Kahawa na ufuta kwenye mikoa ya Songwe na Mbeya ikiwa ni muendelezo wa jitihada za benki hiyo kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kupitia uchumi jumuishi unaochagizwa na huduma rasmi za kifedha.
Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw. Mbwana Kambangwa, huku pia ikihushisha uwepo wa wadau mbalimbali wa sekta za kilimo na ufugaji kutoka mikoa hiyo miwili wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika vya wakulima na wafugaji (AMCOS), pamoja na wadau wengine wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hiyo muhimu.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa aliwaongoza maofisa wengine wa benki hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo inayotoa fursa kwa wakulima na wafugaji wa mikoa ya Songwe na Mbeya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki na kompyuta mpakato ‘Laptops’
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw Kambangwa pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa jitihada zake endelevu zinazolenga kuwasaidia wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini ukiwemo mkoa wa Songwe, alisema ujio wa kampeni hiyo kwenye mikoa hiyo utasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wa wadau mbalimbali wa sekta hizo hususani kupitia huduma mbalimbali za kibenki zilizobuniwa mahususi kwa makundi hayo ikiwemo elimu ya kifedha na huduma za mikopo rafiki.
“Ubora zaidi wa kampeni hii unaonekana pale inapohusisha utoaji wa elimu ya nidhamu ya fedha miongoni mwa wakulima mmoja mmoja na vyama vya ushirika hatua ambayo itawajengea uwezo wa kuona umuhimu wa kujiwekea akiba, umuhimu wa kutumia bima mbalimbali ikiwemo bima ya afya, bima za kilimo pamoja na kuwekeza kwenye zana za kisasa za kilimo.’’
“Hatua hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuhamasisha wakulima wetu kugeukia huduma rasmi za kifedha na hivyo kuchochea uchumi jumuishi. Hii ni hatua kubwa sana ikilinganishwa na tulipotoka miaka kadhaa iliyopita ambapo wakulima na wafugaji walikuwa hawaaminiki na taasisi za kifedha kutokana na kutokuwa waaminifu na wengine kutokuwa na dhamana.’’ Aliongeza.
Akifafanua zaidi kuhusu kampeni hiyo inayotarajiwa kuhitimishwa Juni 15 mwaka huu, Bw Urassa alisema walengwa wa kampeni hiyo ni wakulima wa mazao mbalimbali hususani Kahawa na Ufuta kupitia vyama vya msingi, vyama vikuu vya ushirika na mkulima mmoja mmoja ambao wanahudumiwa na benki hiyo.
Kwa mujibu wa Bw Urassa, ili mkulima mmoja mmoja ashinde zawadi ya pikipiki anatakiwa kwenye akaunti yake awe na fedha kiasi kisichopungua Mil 5 na kwa upande wa AMCOS na vyama vikuu vya ushirika zinatakiwa kuhifadhi kwenye akaunti zao za NBC Shambani fedha kuanzia kiasi cha Sh. Mil 5 hadi mil 50 ili kujishindia laptop na kuwa na fedha kwenye akaunti zao kiasi kisichopungua Sh. Mil 50 ili kujishindia pikipiki.
“Lengo la kampeni hii ni kuwahamasisha wakulima na wafugaji kutunza fedha zao kwenye mifumo rasmi ya kifedha hasa benki badala ya kutunza kwenye mifumo isiyo rasmi. Tunawakaribisha sana kufungua akaunti zao za NBC Shambani ili wawe kwenye nafasi ya kushinda zawadi hizi’’ Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao, Makamu Mwenyeki wa AMCOS ya Mwanjelwa, iliyopo wilayani Mbozi, Bw Imani Luvanda alisema kwa kiasi kikubwa wakulima wilayani humo wamekuwa wakiumizwa sana na gharama za makato ya uendeshaji wa akaunti zao za benki pamoja na kufungwa kwa akaunti zao pindi zisipotumika kwa muda kitu ambacho kimekuwa kikisababisha wengi wao kupoteza imani na matumizi ya taasisi rasmi za kifedha.
“Ila sasa kilichotuvutia zaidi kwenye akaunti hii ya NBC Shambani ni kwamba haina makato yoyote ndio kwanza mkulima anapata faida na zaidi haifungwi kiurahisi hadi ipite miaka miwili.Hii kwetu ni habari njema na binafsi takuwa balozi wa kuwaelimisha wenzangu kuhusu kampeni hii na faida za akaunti ya NBC Shambani’’ alisema.

Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, (alieshika mkasi) akijipongeza sambamba na wadau wengine mara baada ya kuzindua kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe. Wengine ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (katikati) na wadau mbalimbali wa kilimo kutoka mikoa ya Songwe na Mbeya.

Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, (katikati) sambamba na wadau wengine wakionesha zawadi za pikipiki na kompyuta mpakato ‘laptops’ zitakazotolewa kwa washindi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe. Wengine ni pamoja na Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (wa pili kulia) na wadau mbalimbali wa kilimo kutoka mikoa ya Songwe na Mbeya.

Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Songwe Bw Joseph Jerome (kushoto) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Songwe Bw Daniel Msyaliha (kulia) akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo wakiwemo wakulima na viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na benki ya NBC mahususi kwa wakulima mazao mbalimbali ikiwemo kahawa na ufuta katika mikoa ya Songwe na Mbeya iliyofanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe.

Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo ilifanyika mapema jana kata ya Mlowo, wilayani Mbozi mkoani Songwe ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbozi Bw Mbwana Kambangwa, huku pia ikihushisha uwepo wa wadau mbalimbali wa sekta za kilimo na ufugaji kutoka mikoa hiyo miwili wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na vyama vikuu vya ushirika vya wakulima na wafugaji (AMCOS), pamoja na wadau wengine wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa sekta hizo.
No comments:
Post a Comment