Matukio : Makamu Mwenyekiti INEC Atembelea Mafunzo ya Waendesha BVR Pemba - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Sunday 6 October 2024

Matukio : Makamu Mwenyekiti INEC Atembelea Mafunzo ya Waendesha BVR Pemba


Makamu Mwenyekiti  wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk (kushoto) akimsikiliza Afisa wa Tume kutoka Idara ya TEHAMA na Daftari, Lazaro Madembwe aliyekua akimpa ufafanuzi wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete  Mkoa wa Kaskazini Pemba  Oktoba 5, 2024 katika siku ya pili ya mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar ambapo Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. (Picha na INEC).
Makamu Mwenyekiti  wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akifurahia jambo wakati alipotembelea kituo cha mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Micheweni  Mkoa wa Kaskazini Pemba Oktoba 5, 2024 katika siku ya pili ya mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar ambapo Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni. (Picha na INEC).

No comments:

Post a Comment