RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE) amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Dickon Mitchell, Waziri Mkuu wa Grenada, Jijini New York, Marekani.
Katika mazungumzo yao, Mwenyekiti wa GPE ameahidi kushirikiana na Visiwa vya Grenada ili kupatia ufumbuzi hitaji la elimu kwa njia ya mtandao (digital learning) ambalo taifa hilo linahitaji kuwezesha upatikanaji wake kwa wanafunzi wa elimu msingi (basic education) yaani, chekechea, msingi na sekondari.
No comments:
Post a Comment