Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua Rasmi Huduma za Usafiri wa Treni ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam - Morogoro hadi Dodoma, katika eneo la Stesheni Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Pugu Jijini Dare es Salaam wakati akielekea Dodoma kwa Usafiri wa Treni ya Kisasa ya (SGR). Mhe. Rais Dkt. Samia amezindua Rasmi huduma za Usafiri wa Treni ya Kisasa (SGR) kuanzia eneo la Kilometa 0 Stesheni Jijini Dar es Salaam- Morogoro hadi Dodoma tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua safari za Treni ya Kisasa (SGR) kuanzia eneo la Stesheni Kilometa 0 Jijini Dar es Salaam hadi Dodoma tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa mara baada ya kuwasili Stesheni ya Treni ya Kisasa (SGR) Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akinyanyua juu Bendera na kushusha chini (Flag off) kuashiria uzinduzi rasmi wa safari za Treni ya Kisasa ya Umeme (SGR) katika eneo la Kilometa 0 Jijini Dar es Salaam hadi Dodoma tarehe 01 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua jengo la Stesheni ya Treni ya Kisasa (SGR) katika eneo la Kilometa 0 Jijini Dar es Salaam tarehe 01 Agosti, 2024.
No comments:
Post a Comment