Kitaifa : Rais Dkt. Samia Azungumza Na Wananchi Wa Wilaya Ya Mlele Mkoani Katavi - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

13 Jul 2024

Kitaifa : Rais Dkt. Samia Azungumza Na Wananchi Wa Wilaya Ya Mlele Mkoani Katavi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia anaendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mlele katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi mara baada ya kukikagua tarehe 13 Julai, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia anaendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.

Sehemu ya Wananchi wa Mlele waliohudhuria Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wilayani hapo tarehe 13 Julai, 2024.

Shamrashamra za Wananchi wa Mlele wakati wa mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Wilayani hapo katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024.

No comments:

Post a Comment


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633