Biashara : Unaweza Kupata Leseni ya Kawaida, Usajili kokote ukiwa Hata kitandani - BRELA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday 19 June 2024

Biashara : Unaweza Kupata Leseni ya Kawaida, Usajili kokote ukiwa Hata kitandani - BRELA

Na Said Mwishehe, Michuzi TV -Morogoro

KATIKA kuhakikisha wanaendelea kurahisisha utoaji huduma Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umesema kupitia mfumo wa kimtandao wa ORS unaoweza kupata huduma zao zikiwemo za kufanya sajili za kibiashara kama leseni ya kiwanda au kusajili ukiwa kokote kule hata kama utakuwa kitandani.

Hayo yamesemwa na Endrew Mkapa ambaye ni Mkurugenzi wa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni alipokuwa akitoa wasilisho la Leseni za Viwanda pamoja na usajili ambapo amesema kupitia Mfumo wa mtandao unaweza kupata Leseni au kusajili kiwanda ukiwa mahali kokote hata ukiwa nyumbani.

"Kupitia Mfumo wa kimtandao ambao BRELA tunao tumerahisisha sana katika kupata huduma zetu, hakuna haja ya kuja ofisini maana unaweza kupata usajili wa leseni ya biashara kundi A,kupata leseni ya kiwanda na kusajili kiwanda kidogo kwa kutumia mtandao tu.

"Ukiwa na simu kubwa yenye uwezo basi utaingia katika Mfumo wa BRELA na kufanya usajili,kikubwa ni kuwa na viambatanisho muhimu ambavyo vinahitahijika pamoja na aandiko linalohusu kiwanda husika,"amesema na kusisitiza Viwanda vikubwa na vya kati vinapewa leseni na Viwanda vidogo vinasajiliwa.

Amefafanua kuwa viambatanisho ni utambulisho wa mmiliki ambapo atatakiwa kuwa na nyaraka au hati mbalimbali ambazo zinaelezea eneo husika ambalo kiwanda kitakuwepo,uwezo wake kimtaji kwa maana ya uwekezaji na hivyo vyote vitaonekana kupitia andiko na nyaraka nyingine ambazo zitakuwa zimetolewa na taasisi nyingine.

Akizungumza kuhusu leseni ya viwanda amesema Viwanda vimegawanyika katika makundi mawili kwa mujibu wa Sheria ambapo kundi la kwanza ni viwanda vikubwa na vya kati ambavyo mtaji wake unaanzia Sh.milioni 100 na kundi la pili linahusisha viwanda vidogo ambavyo mtaji wake uko chini ya Sh.milioni tano.

Amefafanua ada ya usajili wa leseni ya kiwanda ni Sh.800,000 na ada hiyo inalipwa mara moja tu kwa uhai wa maisha yote ya kiwanda lakini kwa upande wa Viwanda vidogo ada ya usajili ni Sh.10,000 na hiyo ni kwa muda wote.

"Leseni ya viwanda vikubwa ni Sh.800,000 , halafu kiwanda ambacho uwekezaji wake hauzidi hauzidi Sh.milioni ni sh 10,000, uwekezaji ambao unazidi ya Sh.milioni Tano ada yake ni Sh 50,000 na uwekezaji unaozidi Sh.milioni 10 ada yake ni Sh.100,000,"amesema.

Akifafanua zaidi Mkapa amesema kuwa baada ya kiwanda kupewa leseni au kusajiliwa kila mwaka wahusika wanatakiwa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kiwanda ambapo kuna fomu maalum ya kujaza ambayo inauliza maendeleo ya kiwanda.

"Na hii ripoti ya kiwanda ambayo inatakiwa kuwasilisha BRELA kila mwaka haina malipo katika kiwanda .Ni bure kama ukitoa taarifa ndani ya mwaka lakini ukichelewa ndio kuna faini ndogo kama Sh.10,000.

"Lakini tunaamanisha wenye Viwanda ambao wamepata leseni kutoa taarifa zao kwani zinasaidia kutunza kumbukumbu ambazo zinaweza kutumia na Serikali,"amesema na kufafanua ukisoma Ilani ya CCM lakini Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza taasisi za Serikali zisomane badala kuingia katika Mfumo mmoja.

"Hivyo na BRELA tumejiunganisha na mifumo ya taasisi nyingine lakini mfumo huo una matoleo mengine kwa taasisi inayotaka kuingia katika mfumo wetu ili kurahisisha huduma.Hata hivyo BRELA tumejipanga kuendelea kutoa huduma bora sambamba na kuendelea kurasimisha viwanda.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa BRELA wameweka mkakati wao kwamba huduma yoyote ambayo watalifanya haitazidi siku tatu na kama ombi litakuwa limekamilika na hakuna maombi mengi kwa siku hiyo hata saa moja au mbili zinatosha kukamilisha huduma.
4242
4154
4160
4164
4200
4203
4230
4231
4235
4236
4241

No comments:

Post a Comment