Jamii : Wizara ya Maji siyo ya Kulalamikiwa Tena - Waziri Aweso - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Jun 2022

Jamii : Wizara ya Maji siyo ya Kulalamikiwa Tena - Waziri Aweso

Na.Vero Ignatus ,Arusha


Wizara maji imetoa Mafunzo ya Bodi na Menejimenti za Mamlaka za maji safi na usafi wa Mazingira nchini kwa wajumbe 145 na Mamlaka 24, yakiwa na Lengo la kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao ili wananchi waweze kupata huduma Bora.

Akifungua mafunzo hayo jijini Arusha, 29 Juni 2022, Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema, tafiti zinaonesha kuwa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama hupunguza zaidi ya 50% ya magonjwa ya kuambukiza, hivyo kwa kutambua umuhimu huo wa maji kwa afya na maendeleo ya wananchi, Serikali ina jukumu la kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 100.

Uweso amesema maji yana umuhimu wa kipekee katika maendeleo ya binadamu, kiuchumi na kijamii ambapo upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza ni nyenzo muhimu katika kuongeza ubora wa maisha, kupunguza makali ya athari zinazotokana na umaskini na kuongeza kipato cha wananchi.

“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira ni kuboresha utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo husika” Waziri Aweso amesema.

Ameongeza kuwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira ni Taasisi za Serikali zinazojitegemea ambazo zilianzishwa mnamo mwaka 1997 kupitia akaunti maalum chini ya Sheria ya Mwaka 1961(Cap Ordiance 281 Misceleneous Ammendment ACT). Baadae ilitungwa Sheria Na. 12 ya Maji na Usafi wa Mazingira 2009 ambayo iliendelea kuzitambua mamlaka hizi.

Aidha amesema kuwa ,hivi sasa Sheria Na. 5 ya Maji na Usafi wa Mazingira, ya mwaka 2019 ambayo pia imezitambua mamlaka hizo na kuboresha masuala mbalimbali kuziongezea ufanisi. Mamlaka hizo hutoa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika Miji Mikuu ya Mikoa, Wilaya, Miji Midogo na Mamlaka za Miradi ya Kitaifa.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Antoni Sangha amesisitiza Wajumbe wa Bodi kukaa na watumishi wa Idara za maji ili kuweza kuzielewa vizuri na kuweza kuzijua changamoto zinazojitokeza kwa wafanyakazi wa Mamlaka, yatekelezwe kwa wakati na kuchukua hatua stahiki za kinidhamu pale inapobidi 

Sangha amesema kuwa Wizara ya Maji inajitahidi,kwa sasa sio ya kulalamikiwa bali ni kutatua changamoto za maji nchini.amesema kama vile matakwa yanavyowadai kwamba ifikapo 2025 ni kuhakikisha vijijini wanapata maji 85%huku mijini wakioatiwa maji kwa 95% 

"Bodi za maji hakikisheninmnakuwa mnafanya vikao vinavyohitajika kwa wakati,tambueni changamoto zinazojitokeza,chukueni hatua stahiki haswa za kinidhamu pale inapolazimika" alisema Sangha

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Idara ya usambazaji wa Maji safi na usafi wa Mazingira Wizara ya maji Joyce Msiru, amesema Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa masuala mbalimbali yatakayofuata dira ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya wakurugenzi na menejimenti,katika kuzisimamia na kuziendeaza Mamlaka za maji safi na usafi wa Mazingira, ili wananchi waweze huduma Bora na endelevu.

"Hapo awali Wizara ilifanya sema kuwa hapo awali Wizara ilifanya Mafunzo wa bodi ya wkaurugi wa Mamlaka za maji safi na mazingira nchini katika Kanda tatu ikiwemo Njombe,Arusha na Mwanza ambapo Mamlaka 37 Kati ya 70 zilihudhuria na kupata Mafunzo hayo kutokana namichango kutoka Mamlaka zilizohudhuria 

Joyce amesema Wizara ililazimika kuandaa Mafunzo hayo ya siku tatu Jijini Arusha ambapo awali hawakuoata nafasi ya kuhudhuria ambapo yanajumuisha baadhi ya wajumbe wapya wa Bodi na Menejimenti za Mamlaka za Maji safi na usafi wa Mazingira mijini.

Akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wa Bodi za Maji Mwenyekiti wa Bodi ya maji ya Mamlaka ya maji safi na Maji taka jijini Arusha Dkt. Richard Masika amemuhakikishia waziri kuwa kutokana na mafunzo hayo wana uhakika wa kwenda kuzisimamia Mamlaka hizi vizuri na kwa kutimiza majukumu yao bila kusukumwa na kwa weledi mkubwa.

Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza katika Mafunzo ya bodi na menejimenti za Mamlaka za maji safi na usafi wa Mazingira nchini yaliyofanyika Jijini Arusha katika hoteli ya corridor spring 29/6/2022
 Katibu mkuu wa Wizara ya maji John Sangha akizungumza katika Mafunzo ya bodi na menejimenti za Mamlaka za maji safi na usafi wa Mazingira nchini yaliyofanyika Jijini Arusha katika hoteli ya corridor spring 29/6/2022
Mkurugenzi mtendaji wa Idara ya usambazani wa Maji safi na usafi wa Mazingira Wizara ya maji Joyce Msiru akizungumza katika Mafunzo ya bodi na menejimenti za Mamlaka za maji safi na usafi wa Mazingira nchini yaliyofanyika Jijini Arusha katika hoteli ya Corridor spring 29/6/2022

 Baadhi ya wajumbe 145 walishiriki katika Mafunzo ya bodi n amenejimenti za MAmlaka za Maji safi na Usafi wa Mazingira nchini uliofanyika Jijini Arusha 29 juni 2022 katika hoteli ya Corridor spring Jijini Arusha

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad