Habari : Wanahabari Wachanjwa ,Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 13 August 2021

Habari : Wanahabari Wachanjwa ,Dar

 


Mwandishi wa Habari wa TBC Jane John akipata chanjo ya UVIKO 19 leo

Mwandishi wa Habari Zuhura Ally akipata chanjo

  

Na John Mapepele, WHUSM


Wanahabari, wanamichezo na wasanii wameendelea kumiminika leo, Agosti 12, 2021 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya zoezi la hiari la kupata chanjo ya UVIKO 19. Zoezi hili limeratibiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya. 

Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Dkt. Hassan Abbasi, alifafanua kwamba makundi hayo yamependekezwa kupewa kipaumbele na Serikali kwa kuzingatia, pamoja na mambo mengine, umuhimu wao kwa jamii na ukweli kwamba kwa mazingira ya kazi zao, wako katika hatari ya kuambukizwa.

“Zoezi hili ni la siku mbili Agosti 12-13, 2021 Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu (03:00) asubuhi, natoa wito kwa wadau wote kwa hiari yao watumie fursa hii iliyotolewa na Serikali ili wajikinge na wawakinge wengine na UVIKO-19” ameongeza Dkt. Abbasi.

Dkt. Abbasi ameendelea kuwasihi wale waliokosa kujiandikisha awali wawe Wasanii au Wanahabari au Wanamichezo waendelee kuwasiliana kupitia namba 0654063274 au barua pepe matiko.mniko@basata.go.tz  ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA). 

Amesisitiza kuwa Wasanii walio nje ya Dar es Salaam wataendelea kutumia utaratibu unaoendelea kutangazwa na Wizara ya Afya.

No comments:

Post a Comment